Chuo Kikuu cha Durham, Stockton on Tees, UK - (UDUR)

du_2-col_lrg

Durham University (UDUR) ni Chuo Kikuu cha tabaka la juu  ambacho kiko katika sehemu mbili: mji wa Durham, UK, na chuo cha Queen's kilichoko Stockton.Chuo Kikuu hiki ni cha ’collegiate.’ Masomo yake na taratibu zake za utafiti hupeanwa kupitia idara 25 zilizoko katika vitovu vitatu vya chuo kikuu: fani na masomo ya sanaa, sayansi, sayansi ya jamii na afya. Zaidi ya wanafunzi 15,000 wamesajiliwa katika chuo kikuu (3,500 wakiwa wanaosomea uzamili na zaidi ya 3,000 ni wanafunzi wa kimataifa kutoka mataifa 120) na wafanyakazi zaidi ya 3,000. Chuo hiki huwa na mapato ya milioni 160 kwa mwaka.

Wolfson Research Institute (WRI) ni sehemu mojawapo ya Chuo Kikuu cha  Durban ambacho hujihusisha na utafiti juu ya afya ya binadamu na hali njema ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea na kuboresha afya na ubora wa Afya ya watu ikichangia mashauri ya jami, huduma ya wataalamu na ufanisi wa mazao mapya na vifaa. Kufuatia kuanzishwa kwa bodi ya afya ya Chuo Kikuu mwaka wa 2005, WRI imekuwa sehemu ya utafiti.Taasisi hii imeendelea kuongezea shughuli zake katika utafiti wakati vikundi vingine vya utafiti vinaungana na taasisi hii. Vikundi hivi viko katika idara ya anthropolojia na chuo cha biolojia na sayansi za biolojia.Kunao takribani watafiti 150 wanaosaidia katika utafiti na wanafunzi 100 wa uzamili wanaofanyakazi katika WRI.

Mark Booth ni mkurugenzi mshirikishi wa WRI. Ana ujuzi wa epidemolojia unaohusisha paracitolojia.Hii ni jinsi moja ya kuhusisha tafiti za nyanjani (hasa katika Afrika) ikiwa na tathmini za data, ikiangazia mahusiano mbalimbali ili kuleta ufahamu ambao ungebakia umefichika.Utafiti unaweza kuhusisha elimu ya kingamaradhi, elimu kuhusu vimelea, ekolojia na jenetiki ukiwa na lengo la kuelewa kwa undani jinsi magonjwa utokea.Akiwa imeshikilia jukumu lake la masomo ya epidemolojia ya vimelea; Mark amepanua uwanja wake wa utafiti. Sasa hivi anajihusisha na miradi ya aina nyingi inayohusisha wahamaji wa Bangladeshi, jukumu la fani ya hali njema ya wabaleghe, matumizi ya huduma za afya ya mdomo katika jamii zilizoachiliwa huko Uingereza, na kuboresha kufikia huduma za wale hawajawahi kuajiriwa.Mkurugenzi mshirikishi wa WRI, Mark amehusika kwa karibu kufanikisha lengo la shirika. Mark hujumuisha kikundi cha ‘Africa Regional Interest’ kilicho ndani ya WRI ambacho uunda mikakati inayoleta pamoja vyuo vikuu ulimwenguni.

Katika mradi wa Afya Bora ya Baadaye, wafanyakazi wa UDUR wana jukumu la: kutahini matokeo ya mabadiliko ya mazingira kuhusu kuibuka na kusambaa kwa kichocho katika sehemu ya utafiti. Mark Booth anajukumu la kusimamia somo la udaktari wa falsafa uliofadhiliwa na mradi huu, na ni mshiriki wa WP3.
Read 5785 times
Translate