WP6

WP6 –Washika dau wanavyojihusisha na kujiwezesha kupitia kugawanya maarifa na mafunzo

Mfadhiliwa anayeongoza: TCD

Madhumuni

  • Kuwatambua na kama ni muhimu kuwaweka kwenye vikundi, washika dau na kulenga watakaofaidika kutokana na mradi wa Afya Bora ya Baadaye
  • Kuwajulisha watu wote, ikiwemo waliopo sekta za wanasayansi, za wanyama na za afya ya umma kuhusu madhumuni ya mradi huu na kazi za mradi
  • Kuweka vifaa  vinavyofaa vya  kueneza  maarifa  wakati  mradi huu utakapokuwa unaendelea
  • Kuhakikisha mawasiliano yanayofaa baina ya washika dau na watakaofaidika kutokana na mradi huu na pia kusimamia hafla zinazolenga suala ya afya na mabadiliko ya tabia ya nchi katika kongomano la 8 la Ulaya linalojihusisha na madawa ya sehemu zenye joto na afya za kiulimwengu,litakalofanyika 2013, na warsha ya Afrika/Ulaya huko NUR, Rwanda, itakayolenga kuunganisha uigaji wa mabadiliko katika tabia ya nchi (marekebisho na sera)pamoja na wataalamu wa afya., hasa wale wanaohusika na magonjwa yale matatu yaliyolengwa na mradi huu, ili kuweza kutumia matokea ya utafiti huu katika maeneo mengine ambayo uweza kuwa hatarini na kukabiliwa na magonjwa mengine,kama vile Ulaya
  • Kukusanya, kuvumisha (lugha,maneno,muundo wa maandishi) na kuwasilisha maarifa mapya yatakayotokana na mradi huu kwa watakaofaidika  katika miundo na vyombo vya habari vitakayowezesha  utumiaji wa maarifa haya kama ipasavyo
  • Kupeana masomo kwa washiriki wa mradi (wakiwemo wanafunzi wa shahada ya uzamili kwa njia ya utafiti), washika dau walioko na wale watakofaidika na mradi

Kazi:

Kazi 6.1. Kuwatambua. na kama ni muhimu kuwaweka kwa vikundi, washika dau na kulenga watakaofaidika kutokana na mradi wa Afya Bora ya Baadaye

Kazi 6.2 Uenezaji wa kijumla

Kazi 6.3 Uenezaji  uliokusudiwa

Kazi 6.4 Mawasiliano na matokeo

Kazi 6.5 Kukusanya na kuweka pamoja maarifa yote yaliyotokana na mradi na kutafsiri (katika kiwango kinachofaa, lugha,na maneno) kwa watakaofaidika na mradi huu

Kazi 6.6 Machapisho ya kisayansi ya utafiti na mawasilisho katika kongomano za kisayansi

Kazi 6.7 Kujihusisha na warsha za mafundisho (ili kurekebisha vifaa vya kusaidia kutoa uamuzi uliopo WP5

Kazi 6.8 Warsha ya Ulaya na Afrika
Read 4371 times Last modified on Donderdag, 28 Julie 2011 16:23
Translate