Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo, Nairobi, Kenya - (ILRI)

ilri logo

Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo(ILRI) ni shirika lisilokuwa la kufaidi na lisilo la kiserikali likiwa na makao makuu  Nairobi, Kenya, na kituo kingine cha pili  kikiwa Addis Ababa, Ethiopia. ILRI uajiri zaidi ya wafanyakazi 700 kutoka nchi 40, ikifanya kazi katika nyanja za mifugo na umaskini, ikileta sayansi ya hali ya juu na uwezo wa kujenga ili kuweza kupunguza umaskini na kuwa na ufanisi unaowezekana.Kazi ya ILRI hujumuisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali ili kuongezea ujuzi kutokana na washiriki wengine wanaojijumuisha na swala la utafiti wa mifugo.ILRI hutumia utaratibu wenye uvumbuzi ili kuongezea nguvu utafiti wake.Mabadiliko ya kwanza ya utamaduni lazima yakubaliane na mabadiliko ya teknolojia ili kuhimili uvumbuzi katika viwango vyote, kutoka kwa wafugaji wa kibinafsi hadi wale wa  kitaifa na kimataifa wanaotoa uamuzi.Mpango wa ILRI hunuia kutumia mifugo kama kifaa chake cha maendeleo.ILRI imefadhiliwa na mashirika zaidi ya 60 yakiwemo ya kibinafsi,ya umma na pia ya serikali.

An Notenbaert ni mtaalamu wa kupanga namna ya kutumia ardhi akiwa na ujuzi wa utafiti na maendeleo (R&D) wa miaka 15 nchini Belgium na Afrika.Hivi sasa anafanya kazi kama mtafiti katika mradi wa ILRI ya mchanganuo wa "sustainable livestock futures".Kazi yake huangazia taratibu za maarifa ya uchanganuzi juu ya umaskini na mazingira akiwa anajishughulisha na mabadiliko katika tabia za nchi.

Patrick Kariuki ni mwanasayansi wa arthi na mtaalamu wa teknolojia ya ‘geospatial’ aliye na ujuzi wa zaidi ya miaka 17 ya kufanya kazi ya utumizi wa hii teknolojia katika ukadriaji wa raslimali ya arthi na sayansi ya mifugo. Alianza kufanya kazi yake na kuhusika na ramani za arthi, matumizi ya arthi, kupanga matumizi ya arthi, kutathmini arthi, kukadiria mazao, na kutoa ramani juu ya raslimali.Pia amejihusisha na utaratibu wa maonyo ya mapema.Yuko na shahada ya udaktari wa falsafa katika matumizi ya utambuzi kwa umbali na ameandika mengi kuhusu eneo hili la somo lake.

Bernard Bett hufanya kazi ya elimu ya magonjwa ya mlipuko baina ya mifugo katika taasisi ya ILRI.Ana ujuzi katika kuchunguza namna mbalimbali za kuweka mikakati ya kuingilia kati, na hapo awali alifanya utafiti juu ya epidemolojia kati ya wafugaji wa Kisomali na Kiturukana ili kutathimini mgongano katika afya ya mifugo ikiwemo homa ya bonde la ufa. Yuko na shahada ya uzamili wa sayansi na shahada ya udaktari wa falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

Jeffrey Mariner hufanya kazi ya elimu ya magonjwa ya mlipuko baina ya mifugo na ana ujuzi wa miaka 20 katika uzuiaji wa magonjwa, ukaguzi na utafiti barani Afrika na Asia.Amekuwa akijihusisha na namna huduma za afya ya mifugo hupeanwa na ukaguzi wa magonjwa. Alipata shahada ya udaktari wa falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Guelph iliyohusu vielelezo vya ugonjwa unaoambukiza wa sotoka unaoathiri ngombe, na ugonjwa wa nimonia unaoambukiza yavuyavu za ng’ombe.

Watafiti wa ILRI watajihusisha na usimamizi na uchanganuzi data, katika utafiti kati ya uhusiano baina ya mazingira na homa ya bonde la ufa  na katika maendeleo na uwazilishaji wa vifaa vya huhimili wa maamuzi.Wafanyakazi wa ILRI watapeana usimamizi kwa wanafunzi wawili wa utafiti (mmoja wa shahada ya udaktari wa falsafa na mwengine wa shahada ya uzamili wa sayansi) uliofadhiliwa na mradi huu.
Read 16009 times
Translate