Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Rwanda Butare, Rwanda (NUR)

nur

Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Rwanda Butare, Rwanda (NUR), kilianzishwa mwaka wa 1963 na muungano wa serikali ya Rwanda na kikundi cha Dominicana kutoka mkoa wa Quebec (Canada). Mwaka wa 2005, chuo kikuu hiki kilikuwa na wanafunzi 8221 na waathiri 425.

Center for Geographic Information Systems and Remote Sensing (CGIS) kilianzishwa mwaka wa 1999 kupitia makubaliano kati ya NUR na Dian Fossey Gorilla Fund International.CGIS ilishika mizizi ndani ya NUR kama idara mwaka wa 2001.Kikundi hiki kilichochanganyika cha GIS, RS, ICT, ‘webmapping’,mazingira, usimamizi wa miradi, wataalamu wa kifedha na usimamizi,wameweza kufaulu sana katika miaka iliyopita.Kufaulu huku kumefanya watuzwe tuzo la  "Mafanikio Maalum katika GIS" wakiwa kwenye kongomano la 26 la USRI lililokuwa mjini San Diego, California.

Vivien Munyaburanga ni mhandisi aliye na shahada ya uzamili katika mipango ya miji na sehemu zilizokaribiana na hujihusisha zaidi na usimamizi wa miundombinu ya mijini.

Jean Pierre Bizimana ni mwanajiografia aliye na shahada ya uzamili katika usimamizi na mipango ya miji.

Elias Nyandwi ana shahada ya uzamili katika sayansi ya ‘Geo-Information’ na uchunguzi wa arthi.

Watafiti wa CGIS-NUR watajihusha na: WP 1:usimamizi wa miradi ( watu 7 kwa mwezi), WP2:taarifa za magonjwa na ujenzi wa hifathidata(watu 16 kwa mwezi),NUR ni kiongozi wa Kazi 2.3:Maendeleo ya arthi/ matumizi ya arthi/ mandhari/na hifathidata ya maji ya juu ; Kazi 2.5 Kuleta pamoja hifadhidata ya maeneo yanayokaribiana ili kutumika katika kutathimini magonjwa; Kazi 2.7 Kutengeneza hifadhidata ya mtandao wa miradi (mahali pa kuweka taarifa); WP4: magonjwa yanayohatarisha na mitindo ya magonjwa (watu-54 kwa mwezi).NUR ni kiongozi wa Kazi 4.1 Kutambua sehemu zinazodhurika kwa sasa na magonjwa yale matatu yanayolengwa; Kazi 4.3: kupeana mabadiliko ya matumizi katika arthi; Kazi 4.4: Kutoa habari inayoonyesha mabadiliko katika shughuli za kijamii na kiuchumi; Kazi 4.6; Kudhihirisha hatari zinazoweza kutokana na magonjwa na sehemu zinazoweza kukabiliwa na magonjwa haya. ; WP6: Washika dau wanavyojihusisha na kujiwezesha kupitia kugawanya maarifa na mafunzo (watu -2 kwa mwezi). NUR ni kiongozi wa Kazi 6.8: warsha ya pili ya Afrika na Muungano wa Ulaya; WP7: Kuhimiza nguvu za utafiti na matumizi. NUR ni kiongozi wa kazi nne zilizoko WP7.

NUR ni mshiriki mmojawapo katika penali ya wataalamu itakayohakiki mradi inayowakilisha mradi wa Afya Bora ya Baadaye.

Read 22190 times
Translate