AquaTT, Dublin, Ireland - (AquaTT)

aquatt mark


AquaTT ni taasisi ya kimataifa ambayo hupeana huduma za masomo na usimamizi wa miradi ili kuhimilisha maendeleo endelevu katika maliasili majini mwa Ulaya. AquaTT hufanya kazi ya kuunganisha maarifa kati ya utafiti na maendeleo katika mazingira na katika sekta ya biashara.  AquaTT imekuwa, kwa miaka kumi na saba sasa, ikijihusisha na kusimamia miradi ya Muungano wa Ulaya  na imekuwa na uwezo wa kutoa huduma katika miradi ya utafiti, ikwemo; usimamizi wa miradi, mawasiliano, uenezaji, mafundisho, na teknolojia na upashanaji wa hekima kwa wanaolengwa.  

David Murphy ni msimamizi mkuu wa AquaTT  kwa miaka 9 akiwa akifanya kazi katika miradi ya  Muungano wa Ulaya katika uwanja wa elimu, na RTD, akiwa ameratibu miradi 9 na kuhusika na miradi zaidi ya 25. Mbali na hayo ameratibu mmojawapo ya makundi ya kielimu yanayohusika na ‘Aquaculture’, Fisheries and Aquatic Resources’, AQUATNET (2000-2005) na imesaidia kupanua makundi hayo ili kujumuisha ujuzi na kuelimika na kuweza kutatua changamoto  huko  Bologna na  Copenhagen. AquaTT itaendelea na kusimamia huduma za makundi ambayo yameratibiwa na Chuo Kikuu cha Gent. David pia amekuwa akiendesha sehemu ya hekima ya usimamizi wa masomo katika sehemu ya Ulaya ya teknolojia ya ‘Aquaculture’ and Innovation Platform (EATIP). Ujuzi wake utahakikisha kuwa mawasiliano na shughuli za uenezaji katika Mradi  wa Afya Bora ya Baadaye umekuwa uzoefu unaohakikisha kuna matokeo yanayopimika kwa wanaolengwa na wanaoutumia.

Paul Lowen ni mwanasayansi wa kimazingira aliyechukuliwa na AquaTT kama ofisa wa mradi atakayekuwa hasa katika mradi wa Afya Bora ya Baadaye. Hapo awali alifanya kazi katika elimu ya mbuga za wanyama na wanyama wa porini huko Ayalandi, kazi ambayo ilifanya ufanisi na kutoa taratibu za elimu kwa shule na makundi ya jamii. Anayo shahada ya biolojia ya mazingira na shahada ya uzamili katika uhifadhi wa mifumo ya ikolojia na usimamizi wa ardhi.

Katika mradi wa Afya Bora ya Baadaye AquaTT itakuwa na wajibu wa kusimamia na kuongoza mradi, ikiongozwa na WP 1, ikiunga mkono mratibu wa mradi huu (Professor Taylor).Na kwa vile  AquaTT na shirika linaloongoza  Afya Bora ya Baadaye (TCD) huwa Dublin, mikutano ya ana kwa ana ya kuonyesha kunavyoendelea itawezekana. AquaTT itaongoza pamoja na WP 6 ‘Kugawanya masomo na kupitisha hekima’, ugawanyaji wa jumla wakitumia huduma za AquaTT ili kuhakikisha kuna utambuzi na ugawanaji wa kidesturi kwa watakaofaidika. AquaTT itajihusisha na WP 7 katika Kuhimiza nguvu za utafiti na matumizi, kupanga ordha ya penali za wataalamu wa kukagua mradi wanaohusiana na WP.
Read 9752 times
Translate