Fizikia ya taratibu za Ulimwengu, The Abdus Salam International Centre for Theoretical Physics, Trieste, Italy - (ICTP)

ictp


Fizikia ya taratibu za Ulimwengu, The Abdus Salam International Centre for Theoretical Physics, Trieste, Italy - (ICTP) ilianzishwa mwaka wa 1964 ikiwa na lengo la kukuza utafiti katika sayansi ya asili na hisabati, hasa katika nchi zinazoendelea. Utafiti wa Earth System Physics (ESP) kisehemu cha ICTP kinahusisha mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababishwa na binadamu, tofauti za kawaida zilizopo katika tabia ya nchi, na kubashiri tabia ya nchi katika misimu mifupi hadi muda wa miaka kumi. ESP imeshikilia na kustawisha kielelezo kilichokamilika cha hewa ya bahari za ulimwengu na vielelezo vya tabia ya nchi ya sehemu zilizokaribu. Kuhusiana na wito huu, vielelezo vyote viwili vimetumika ili kutatua shida za utafiti barani Afrika na pia katika baadhi ya vituo vya kiafrika vya utafiti. ICTP pia utafiti juu ya ustadi wa takwimu na jinsi mbinu za utafiti za kiulimwengu na za maenoe ya nchi zaweza kutumika maeneo maalum nchini.ESP hujihusisha na miradi ya sasa ya Ulaya ya ENSEMBLES, CECILIA, WATCH na ACQWA.

Katika mradi wa Afya Bora ya Baadaye, ESP imechukua jukumu la mradi wa Muungano wa Ulaya-FP7 unaoitwa QWECI kuanzia mwaka wa 2010, utakaochunguza uwezekano wa kubashiri kimwezi au kimsimu mlipuko wa malaria, na homa ya bonde la ufa nchini Malawi, Senegal na Ghana. ICTP pia itapata ujuzi wa ufundi unaohitajika ili kujua kinochosababisha magonjwa haya na itapata ujuzi wa kuunganisha pamoja utabiri wa tabia ya nchi na mitindo ya magonjwa. Utafiti huu utanufaisha zaidi mradi wa Afya Bora ya Baadaye (WP2 tabia ya nchi ya sasa, WP3 vielelezo vya mitindo ya magonjwa na WP4, tabia ya nchi ya siku za baadaye) na hii inaonyesha kuwa utafiti uliopendekezwa utaweza kujengeka katika mradi uliopo kwa wakati huu.

Adrian Tompkins (ESP) ataratibu na kuongoza juhudi za ICTP katika mradi wa Afya Bora ya Baadaye, Yeye ni mmoja wa viongozi/ wa waandishi wa QWECI.Alipokea shahada ya udaktari wa falsafa  kutoka  Chuo Kikuu cha Reading, akakaa katika chuo cha utabiri wa hali ya hewa cha Max Planck nchini Ujerumani kwa miaka mitatu na akafanya kazi miaka saba katika kituo kinachojulikana ulimwenguni cha utabiri wa hali ya hewa, ECMWF,kabla ya kujiunga na ICTP mwezi wa Oktoba 2007. Ana ujuzi katika kufanikisha na matumizi ya utabiri wa hali ya hewa ulimwenguni na vielelezo vya tabia ya nchi pamoja na vielelezo vya namna ya kutatua mawingu ya sehemu za karibu.Kazi yake, inayozidi zaidi ya miaka 40 ya machapisho maalum, inahusisha kazi za tabia ya nchi barani Afrika na utabiri wa tabia ya nchi kama ulivyoigizwa katika badhi ya vielelezo vya hali ya hewa na mbinu za numerali kuhusu tabia ya nchi.

Filippo Giorgi hivi sasa ni mwanasayansi wa ngazi za juu katika ICTP na kiongozi wa ESP, alichojiunga nacho Mei, 1998. Alipata shahada ya udaktari wa falsafa mwaka wa  (1986) katika sayansi ya hali za anga kutoka Chuo cha Tekinolojia cha Georgia na pia akafanya kazi kama mwanasayansi katika National Center for Atmospheric Research (NCAR) huko Boulder, Co, Amerika, hadi mwaka wa 1998. Ni mmoja wa waandishi waliochapisha majarida yanayorejelewa na alikuwa mpelelezi katika vyuo vya utafiti zaidi ya 20 katika bara la Amerika Magharibi na Ulaya.Yeye ndiye aliyeanzisha vielelezo katika uwanja wa tabia ya nchi katika sehemu zilizokaribiana.

Erika Coppola alipokea shahada ya Laurea ya Fisikia (1998) kutoka Chuo Kikuu cha LAquila na shahada  ya udaktari wa falsafa  katika utabiri wa hali ya hewa (2004) kutoka kwa Chuo Kikuu cha Reading, UK, iliyojihusisha na utafiti juu ya utambuzi kwa umbali wa hali ya hewa kutoka anga za juu, ikiwa ikiaangazia hasa kunyesha kwa mvua katika  bara la Afrika. Kutoka mwaka wa 2002 hadi 2006 amekuwa na cheo cha udaktari katika Chuo cha L’Aquila, kisha akafuatia kuwa mtafiti wa kisayansi hivi sasa katika ICTP.Amekuwa akijihusisha na  utafiti wa hydrolojia na juhudi za  ufanisi ikiangazia maarifa juu ya maji barani Afrika.

Watafiti wa ICTP watatumia maarifa yao ya utafiti wa tabia ya nchi katika WP2 na manthari ya tabia ya nchi ya siku za usoni ya WP4.Watashauri WP3.
Read 11221 times
Translate