Idara ya Afya, Uganda (CH)

ch_uganda_cropped


Idara ya Afya, Uganda  ni shirika la serikali ambalo liliundwa ili liwe linaunda sera; kuhakikisha ubora katika kazi; kuratibu tafiti za afya; na kuangalia na kutathmini namna sehemu ya afya inavyofanya kazi. Wizara hii inalenga kuhakikisha kuwa watu wana afya, wanauzalishaji na mali ili kuweza kukuza Afya yenye siha na uzalishaji unaofaa.

Afya ya Jamii Idara ya wizara ya afya Uganda inajihusisha na kukuza afya, kuzuia magonjwa,na mambo ya afya ya kijamii, siha ya mazingira, afya ya shule,pamoja na jinsia na afya.Lengo kuu la idara hii ni kuongezea ufahamu na maarifa juu ya afya na jinsi ya kuzuia magonjwa na kukuza Afya yenye siha ili kuwa na watu wenye siha na uzalishaji nchini Uganda. Ili kufikia haya madhumuni utafiti ni muhimu katika kuunda sera na maamuzi.

Agaba Friday hufanya kazi ya udaktari. Kwa miaka 30 sasa amekuwa na ujuzi katika sehemu za afya za kiraia na kibinafsi, afya ya maishilio na mazingira, tekinolojia ya mazingira na maendeleo endelevu. Kuongezea masomo yake ya udaktari, Agaba ana shahada ya uzamili ya teknolojia ya mazingara (Imperial College, UK) na Diploma kuhusu afya katika viwanda (LSHTM, UK). Alikuwa mmoja wa washiriki katika mradi wa Uganda wa National Adaptation Programmes of Action (NAPA).

Didas Namanya ana shahada ya jiografia na diploma ya elimu (kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda) na vyeti mbalimbali vya ‘Mabadiliko katika tabia ya nchi,kupunguza na marekebisho (kutoka kwa WHO), Arc GIS (ESRI), mabadiliko ya tabia za nchi inavyoonekana Afrika (World Bank),kutathmini umaskini na jinsi unavyohusiana na afya(ILRI), kuchimbua madini, afya na mazingira (MWE-GSM) na mawasiliano ya kisayansi (CDC).Utafiti wake unahusika na mabadilko ya tabia za nchi, usambazaji wa maradhi na mikurupuko ya magonjwa; utaratibu wa kutoa maonyo mapema juu ya maradhi ( tathmini na vielelezo); na uwezo wa urekebishaji wa sekta ya afya ikizingatia mabadiliko ya tabia za nchi.Didas ni mshiriki wa Uganda ‘National Climate Change Policy Committee’ na ‘National Health Information Management System and Integrated Disease Surveillance and Response Committee’.Pia ni mshiriki wa National Adaptation Programmes of Action (NAPA) mradi wa mabadiliko ya tabia za nchi na hivi sasa ni mmoja wa washiriki wa ‘East African Integrated Disease Surveillance Network’ (EAIDSNet).

Wanaoshiriki katika idara ya CH watatoa mchango wao katika WP 2, 4, na 6 katika majukumu waliyopewa katika ushauri ulioko kwenye bajeti.Wanaofanya kazi huko watafanya utafiti na kuhusika na kuhamisha vifaa vya kuhimili maamuzi kwa washika dau, kupitia kwa warsha ya WP6. Kundi hili litatumia ujuzi wake ili kuchangia katika maendeleo ya utaratibu wa kutoa maonyo ya mapema katika kuangazia magonjwa na vifaa vya kupunguza na urekebishaji wa mabadiliko ya tabia za nchi katika sehemu ya afya.

Read 10859 times
Translate