TRAC PLUS (Kituo cha matibabu na utafiti juu ya UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu na maradhi mengine) , Kigali, Rwanda - (TRAC Plus)

trac plus


TRAC PLUS (Kituo cha matibabu na utafiti juu ya UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu na maradhi mengine) Kituo hiki kiko katika wizara ya Afya, Rwanda,na kilianzishwa mwaka wa 2007 ili kuhudumia kama kituo cha kitaifa cha kuzuia magonjwa yanayoambukiza na uzuifu katika Rwanda. Kiliundwa kama muungano kati ya kituo cha zamani cha ‘Treatment and Research AIDS Centre (TRAC)’, National Malaria Control Program (PNILP) na National Tuberculosis and Leprosy Control Program (PNILT).TRAC Plus iliundwa ili kuunganisha juhudi za kupigana na magonjwa yanayoambukiza na hasa ugonjwa wa UKIMWI, magonjwa ya zinaa, Malaria, Kifua Kikuu na magonjwa mengine yanayoambukiza. TRAC Plus iko  chini ya usimamizi wa wizara ya Afya. Ina hali halali, usimamizi na fedha za serikali hivyo basi hutawaliwa kulingana na sheria inayolinda huduma za raia nchini Rwanda.

Sebahungu Fidele hivi sasa ni kiongozi wa kuchunguza epidemolojia katika TRAC-Plus sehemu ya malaria, Wizara ya afya Rwanda. Yeye ni dakitari aliyejihusisha na utafiti na utabibu wa UKIMWI na malaria.

Watafiti wa TRAC Plus hujihusisha zaidi na kutahini matokeo ya mabadiliko ya mazingira kuhusu kuibuka na kusambaa kwa malaria.


Read 14337 times
Translate