Chuo kikuu cha taifa cha Singapore (National University of Singapore –NUS)

nus-logo 


Chuo kikuu cha taifa cha Singapore (National University of Singapore) kikiwa bara la Asia ni mojawapo ya vyuo vinavyoongoza duniani. Chuo hiki kilipewa nafasi katika vyuo 25 bora zaidi ulimwenguni mwakani 2012 kulingani na QS inayotoa nyadhifa za vyuo bora zaidi ulimwenguni (http://www.topuniversities.com/university-rankings/world-university-rankings). NUS ina idara na shule 16 katika kampasi tatu zilizoko Singapore, Kent Ridge, Bukit Timah and Outram. Chuo hiki kina mtalaa ambao unasisitiza masomo kutoka nyanja mbalimbali na wahadhiri mbalimbali. Zaidi ya wanafinzi 37,000 kutoka nchi 100 wanasomea katika chuo hiki na kuchangia katika kuwepo kwa mila, desturi na utamaduni  kwa namna mbalimbali.

NUS ina vituo vitatu vya utafiti ambavyo ni bora zaidi na taasisi na vituo 22 vya utafiti vyenye cheo cha chuo kikuu. Pia ni mshiriki katika Singapore’s 5th RCE. NUS inashirikiana kwa karibu na  taasisi pamoja na vituo 16 vya utafiti. Shughuli za utafiti wa NUS zinalenga kuwa na matokeo muhimu  na NUS inajulikana kwa utafiti wake thabiti katika nyanja za uhandisi, biolojia, udaktari, sayansi ya jamii na sayansi asili. Tafiti kubwa zimefanywa hivi karibuni katika maeneo kadhaa kama vile teknolojia ya kwanta; kansa na utafiti kuhusu namna ya kuboresha afya ya binadumu kwa kutumia mbinu kadhaa, ikiwemo kujumuisha jamii katika juhudi hizo; media wasilianifu na ya dijitali; na mazingira na maji. Chuo hiki pia kinajitahidi kuweka hali ambayo itawezesha watu katika jamii ya NSU kuwa na moyo wa utendaji na watu wenye bidii. NUS ni mshiriki mkubwa katika utafiti wa kimataifa katika nyanja ya kielimu na mitandao ya utafiti kama vile Chama cha Vyuo Vikuu Pacific Rim (APRU) na Muungano wa Kimataifa wa Vyuo Vikuu vya Utafiti (IARU). Hii mitandao ya kimataifa huongezea wadhifa wake wa kimataifa. NUS pia inajulikana kwa  kuhusika kwake katika  miradi ya utafiti iliyofadhiliwa na muungano wa Ulaya.

Idara ya Jiografia katika NUS iko katika Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii na inajumuisha zaidi ya wafanyakazi 30 wa kitaalamu pamoja na wale wanaofanya utafiti. Utafiti katika Idara umegawanywa katika makundi matatu, moja likiwa – Mabadiko ya Mazingira katika nchi zenye joto-inaongozwa na Profesa David Taylor. Idara ya Jiografia sasa (2012) iko katika nafasi ya sita bora duniani katika Nyanja hii kulingana na nyadhifa za QS.

David Taylor alikuwa Profesa wa jiografia katika chuo kikuu cha TCD kuanzia Januari 2001 hadi Septemba 2012. Kuanzia Septemba 2012 amekuwa Profesa anayehusika na Mabadiko ya Mazingira katika  nchi zenye joto, idara ya Geographia, NUS. Utafiti wake mkuu unahusu mazingira katika nchi zilizo na joto, na hasa kwa kiasi gani mabadiliko ya mazingira katika Afrika ya Kati na Mashariki yanahusu binadamu na ekolojia. Akiwa alifanya shahada ya udaktari wa falsafa nchini Uganda mwanzoni wa miaka ya 80, David sasa ana zaidi ya miaka 25 ya uzoefu wa kufanya utafiti katika sehemu hizi na zingine zenye joto.Utafiti mwingi umehusu sehemu zenye unyevunyevu.

Read 4028 times
Translate