Chuo Kikuu cha Liverpool, UK - (UNILIV)

colour_logo_0848

Chuo Kikuu cha Liverpool ni mojawapo ya vyuo vinavyoongoza katika utafiti na mwanachama wa kikundi cha Russell, chenye utafiti wa kiwango cha juu na mapato ya milioni £340 kila mwisho wa mwaka, pamoja na milioni £123 za utafiti.Chuo hiki kimewekwa katika nafasi ya 16 na ‘Times Higher Education’ kwa sababu ya jumla ya tuzo kilichopokea za utafiti na kwa ‘Financial Times’ kikawa kati ya vyuo 10 vilivyotoa utafiti wenye uzalizaji na kupokea fedha za viwanda za ufadhili. Chuo kikuu hiki kilianzishwa mwaka wa 1881 na kupewa chata chake mwaka wa 1903 na kinajihusisha na watu wanane waliopewa tuzo ya Nobeli. Jumla ya asili mia 53 ya wafanyakazi wa utafiti walipewa vyeti vya juu katika vikundi viwili ‘4* (kuongoza ulimwenguni) and 3* (bora zaidi ulimwenguni)’ kwa sababu ya utafiti uliokuwa Uingereza (2008) wa ‘Government Research Assessment Exercise (RAE).’ Kuna wanafunzi 21,000 na 4,900 wanaofanyakazi katika chuo kikuu.

Idara ya Jiografia ina takribani wanafunzi 500 na zaidi ya wafanyakazi 30 wa utafiti wanaohimili Programu 10 za shahada ya BA na BSC, tano za shahada ya uzamili na shahada zingine za udaktari wa falsafa zikiwa na kadri ya wanafunzi 55. Jumla ya asili mia 55 ya watafiti wanaofanya kazi walipewa vyeti vya juu katika vikundi viwili ‘4* (kuongoza ulimwenguni) and 3* (bora zaidi ulimwenguni)’ kwa sababu ya utafiti uliokuwa Uingereza (2008) wa ‘Government Research Assessment Exercise (RAE)’ uliyochapishwa Disemba 2008. Idara hii ina rekodi ya utafiti iliyopewa udhamini kutoka nje kama £2.5m tangu 2001.Ufadhili wa utafiti umetoka halmashauri mbalimbali zikiwemo NERC, ESRC, Charities na Trusts Leverhulme, Welcome Trust na kutoka kwa ufadhili wa kimataifa kama vile Muungano wa Ulaya.

Dr. Andy Morse ni profesa mshiriki (kikiwa ni cheo cha kupandishwa cha utafiti) katika idara ya Jiografia. Shahada yake ya udaktari wa falsafa inahusu Fisikia ya anga za juu. Kwa miaka 15 amekuwa akifanya kazi ya namna ya kutumia taarifa za tabia za nchi ili kuweza kubashiri jinsi mabadiliko ya tabia za nchi yataathiri afya na pia amefanya juhudi kubuni vielelezo kuhusu magonjwa yanayosababishwa na mabadiliko haya.Ameongoza miradi kadhaa inayojihusisha na tabia za nchi (kuhusu kilimo, raslimali za usambazi wa nguvu za umeme, bima zinazohatarisha n.k) lakini hasa kuhusu afya katika idadi kubwa ya miradi kama vile EC FP5 DEMETER, EC FP6 ENSEMBLES, pale ambapo ni mshiriki wa bodi ya menejimenti, EC FP6 AMMA na NERC iliyofadhili AMMA na ni mratibu mkuu wa EC FP7 QWeCI na kiongozi msaidizi wa mradi wa NERC ENHanCE. Andy amekuwa mshiriki wa-PI katika fedha za ufadhili kutoka kwa ‘EC na NERC, Leverhulme, Wellcome Trust na Meningitis Research Foundation.’ Ana ujuzi katika usimamizi wa miradi iliyounganishwa ya Muungano wa Ulaya. Mwaka wa 2006 Andy alikuwa mmoja wa waliopokea tuzo la ulimwengu la ‘World Meteorological Organisation Norbert Gerbier-MUMM’ iliyotokana na jarida lililochapishwa na ‘FP5 DEMETER datasets.’ Sasa hivi anahudumu katika komiti ya kisayansi ya ICSU Earth System Science Partnership (ESSP) mradi wa pamoja wa mabadiliko ya mazingira ya kiulimwengu na afya ya binadamu; WMO ikiwa ni programu ya utafiti wa tabia ya nchi ulimwenguni-World Climate Research Programme (WCRP), CLIVAR kikundi cha kufanya kazi ya kubashiri hali ya tabia ya nchi kimsimi na kimwaka; na WMO WCRP CLIVAR  ambayo ni penali ya kukagua mabadiliko ya tabia ya nchi barani Afrika.

Wafanyakazi wa utafiti katika UNILIV watakuwa na jukumu la; Kuonyesha mitindo ya magonjwa matatu, yaani, malaria, homa ya bonde la ufa na kichocho kama sehemu moja ya WP3.
Read 8752 times
Translate