Taasisi ya Mazingira ya Stockholm, Dar es Salaam, Tanzania (SEI)

sei_logo_491c

Taasisi ya Mazingira ya Stockholm Tanzania ilianzishwa mwaka wa 1989 na serikali ya Uswidi, na ni shirika huru la kimataifa la utafiti ambalo limejihusisha na mazingira na maendeleo ya mitaani, kitaifa, maeneo yaliyokaribu na ya ulimwenguni kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita.Lengo la SEI ni kuleta mabadiliko ya maendeleo yanayokubalika kwa njia ya kuunganisha pamoja sayansi na sera kupitia tathmini ambazo zinahimilisha wanaofanya maamuzi. SEI inajihusisha na tafiti mbalimbali zinazohusiana na mabadiliko ya mazingira ikilenga namna ya kuleta maendeleo kwa kutumia vifaa kama “Knowledge Elicitation Tools” (Knets), kukagua mitindo ya magonjwa na maamuzi, tathmini za kisiri, tathmini zinazolinganishwa, makundi ya jamii, na  vifaa vya kusaidia kutoa uamuzi ili kuchunguza namna ya kuleta urekebishaji kwa kutumia methodolojia tofauti. Kituo cha SEI cha Afrika kipo katika shirika la kukadiri raslimali chuo kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Lengo  la SEI ni kuwezesha  ushirikiano wa karibu na mashirika mengine ya kiafrika  na makundi ya kimazingira ya kiafrika na maendeleo ya mambo mbalimbali. Kituo hiki cha SEI cha Afrika huchukuliwa  kama kituo kinachounganisha Afrika kusini, mashariki na magharibi.

Stacey Noel ni mwanaikonomia wa kijamii anayefanya utafiti kuhusu vile maji, umaskini na maendeleo ya kibiashara yanaathiriana. Stacey alijiunga na SEI Afrika Juni 2005 na kujiunga na ofisi ya uratibu Dar es Salaam, Tanzania mwaka wa 2008. Kazi yake ikiwa ni utafiti, anahudumu kama mkurugenzi wa SEI wa raslimali ya maji na taratibu za maarifa ya usafi. Yeye ana shahada ya uzamili katika usimamizi wa ufanisi kutoka chuo kikuu cha London School of Economics.

Basra Ali ni mmoja wa wanaoleta mweledi katika ufanisi akiwa na zaidi ya miaka 9 ya ujuzi wa kufanya kazi na mashirika ya kushaurisha ya kiulimwengu na taratibu za shirika la ufanisi la UNDP. Basra ana shahada kutoka Chuo Kikuu cha Moi, Eldoret, Kenya na hivi sasa anamalizia shahada ya uzamili kutoka IDS, Chuo Kikuu cha Nairobi.Uthabiti wa Basra umekuwa katika mashauri na kuhusisha wanaoshiriki pamoja na kutathmini wanaoweza kudhurika katika makundi yaliyoathiriwa.
Read 9240 times
Translate