Chuo kikuu cha Cape Town, South Africa - (UCT)

logocircless

Kilianzishwa mwaka wa 1829 kama chuo cha Afrika Kusini, Chuo kikuu cha Cape Town (UCT) ndicho chuo kikuu cha zamani sana Afrika na ni mojawapo ya vyuo vinavyoongoza kwa masomo na utafiti Barani Afrika.UCT ilianzishwa mwaka wa 1918. Hivi sasa, ikiwepo ndani ya jamii inayobadilika kwa kasi na iliyochanganyika, UCT inaanzisha mwongozo wa kubadilisha unaoangazia kuweko kwa wafanyakazi wa namna mbalimbali, usawa kwa wanafunzi, taratibu za masomo, uongozi na utawala na jinsi ya kusimamia chuo hiki na tabia kwa jumla. Jumla ya idadi ya wanafunzi ni 21 562 (15,413 wanaosomea shahada za digrii na 6,149 wanaofanya shahada ya uzamili) mwaka wa 2006.Zaidi ya wanafunzi 4000 ni wa kimataifa wanaotoka nchi 97 tofauti. Kuna zaidi ya wafanyikazi 700 ama T3 wakudumu katika idara sita katika chuo kikuu na chuo cha biashara (GSB). UCT inayo watafiti 23 wa ngazi za juu.

Climate Systems Analysis Group (CSAG) iko katika idara ya mazingira na sayansi ya Jiografia. CSAG ni kikundi cha watafiti wanaolenga mabadiliko ya tabia za arthi. Wananuia kufanya utafiti unaohusika na mabadiliko ya tabia za nchi utakaotumika katika nchi zinazoendelea.Kikundi hiki kilichoundwa mwaka wa 1992, ndicho kikundi kinachoongoza katika utafiti juu wa mabadiliko ya tabia za nchi barani Afrika, na hujaribu kuleta pamoja sayansi na jamii (ambayo mara nyingi huwa yamegawanyika) na kuyaunganisha pamoja na huduma za tabia ya nchi zinazostahiki na vifaa vya kutoa usaidizi vinavyotokana na washika dau. Kikundi hiki kinahusisha washiriki 35, pamoja na wafanyakazi wanaojumuisha; wanasayansi wakuu, watafiti walio katika kiwango cha uzamili, wanafunzi wa udaktari wa falsafa, watawala na wanaowasaidia. CSAG ina mahusiano ya kitaifa na kimataifa na hupeana mawaidha ya kisayansi ya kimataifa na taratibu za sera, ikiwa pamoja na IPCC.

Bruce Hewitson alipewa wadhifa kupitia South African Research Chairs Initiative (SARChI). Anayeongoza utafiti kama huu hutarajiwa kuchangia katika mipango ya Chuo Kikuu na kupeana msingi utakaojumuisha na kupanua utafiti ulio bora.Bruce anaongoza CSAG katika UCT. Hii ni mojawapo ya makundi makubwa ya utafiti ya tabia za nchi barani Afrika ikiwa inalenga mabadiliko ya tabia za nchi kama mojawapo ya changamoto zinazolikumba bara la Afrika.Lengo kuu la utafiti katika CSAG ni kuongezea maelewano ya sehemu zilizokaribiana juu ya mabadiliko ya tabia za nchi na kujenga uhusiano kati ya sayansi na jamii inayofaa. Bruce ni mwana klimatolojia aliye na ujuzi mkuu. Amekuwa hapa UCT tangu mwaka wa 1992. Amehusika na utafiti unaohusisha vielelezo na mabadiliko ya tabia za nchi. Pia anahusika na tekinolojia inayofaa barani afrika na ujenzi wa kisayansi.

Katika Afya Bora ya Baadaye, UCT (CSAG) wanajukumu la: kutathmini na kupeana vurumai la mabadiliko ya tabia za nchi katika eneo linalofanyiwa utafiti kutokana na matokeo ya miradi ya zamani hadi inayoendelea hivi sasa; na kutoa vurumai za hali ya juu za sehemu zinazokaribiana kuhusu tabia za nchi za maeneo yanayofanyiwa utafiti ya Afrika Mashariki (WP4).
Read 7227 times
Translate