Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya - (UoN)

uon logo

Chuo Kikuu cha Nairobi, ushirika ulioanzishwa na sheria ya bunge kifungu cha 210 kulingana na sheria za Kenya, ni chuo kilichotangulia katika masomo ya vyuo vikuu nchini Kenya na maeneo ya karibu.Kimekuwa chuo kikuu cha pekee nchini Kenya kwa muda mrefu,na kimeitikia wito wa kitaifa, maeneo ya karibu na Afrika kutoa masomo ya hali ya juu na kuchagua zaidi masomo ya sayansi, tekinolojia, masomo ya sanaa na sayansi ya jamii na fani.Hadi sasa idadi ya taratibu zinazopeanwa ni kadri ya mia mbili wanafunzi wakiwa wanasomea shahada za digrii ya kwanza na shahada za uzamili,zikiwa na utaratibu uliosimamiwa vizuri. Chuo kikuu hiki pia hupeana nafasi ya kufanya utafiti unaofaa na kituo cha kutoa ushauri.Chuo hiki hujihusisha na taratibu na shughuli za jamii. Kuanzia mwaka wa 2008 chuo hiki kimeithinishwa na ISO (ISO 9001 - 2000 Quality Management System (QMS)).

Shirika la masomo ya taaluma ya maendeleo (IDS), liliundwa mwaka wa 1965, na ni mojawapo ya mashirika ya kitambo na shirika liloanzishwa la utafiti barani Afrika. IDS ni shirika lililochanganyika na lililo na masomo mbalimbali katika chuo kikuu cha Nairobi, chuo cha masomo ya sanaa na sayansi ya jamii. Huangazia mambo ya kiujamii na kiuchumi na namna ya kuendesha ufanisi nchini Kenya, sehemu nyingine za Afrika na ulimwenguni.Shirika hili pia lilianzisha masomo yake na utafiti juu ya mashauri, na hupeana huduma za utafiti kwa serikali, vikundi visivyo vya kiserikali, na mashirika ya kibinafsi. IDS hujijenga kwa uchanganuzi wa ufanisi na hutumia karakana, warsha na majarida ili kuwasilisha na kupata matokeo ya utafiti.IDS pia huhimiza kubadilisha kwa maarifa kupitia ushirikiano wa utafiti na kuwaalika wataalamu wa utafiti.

Winnie Mittulah ni profesa mshiriki katika IDS. Yuko na shahada ya digrii ya kwanza na ya uzamili katika sayansi ya siasa na tawala za watu (zote kutoka kwa Chuo cha Nairobi) na shahada ya Udaktari wa Falsafa kutoka kwa chuo kikuu cha York,UK, (Institute of Advanced architectural Studies). Winnie ni  mtafiti mwenye ujuzi na ametoa machapisho mengi.Kiini cha kazi alizoziandika Afrika Mashariki huangazia utawala, umaskini, ufanisi na usimamizi raslimali(na hasa uvuvi katika maji baridi) na makao ya muda na yasiyokubalika.

Watafiti wa IDS wanajukumu la kutathmini data za kijamii na kiuchumi, makazi na data za uhamaji na sera zinazohusiana na matukio ya mikurupuko ya magonjwa yale matatu yaletwayo na vekta katika sehemu inayofanyiwa utafiti, pamoja na data na sera zinazoonyesha maitikio kutokana na mikurupuko hii.(Kazi 2.1)

Read 12075 times
Translate