Taasisi ya Utafiti wa Matibabu,Nairobi, Kenya - (KEMRI)

kemri

Kenya Medical Research Institute (KEMRI) ni shirika la kiserikali lililoanzishwa kupitia kwa marekebisho ya sheria ya sayansi na tekinolojia ya mwaka wa 1979.Kama shirika la kiserikali lina jukumu la kufanya utafiti wa afya nchini Kenya.KEMRI imekua na kuwa kiongoza katika sehemu zilizokaribu katika utafiti wa afya ya binadamu, na hivi sasa imechukua nafasi bora katika utafiti wa afya barani Afrika na ulimwenguni. Ili kuhakikisha kuwa wanaweza kutatua changamoto za afya, KEMRI imeunganisha shughuli zake za maazimio katika programu inne: magonjwa yanayoambukiza, magonjwa yanayosababishwa na vimelea, epidemolojia, afya ya raia, na utafiti wa utaratibu wa afya; na bioteknolojia pamoja na magonjwa yasiyoweza kuambukiza. Miongoni mwa maagizo yake ni kujihusisha na makundi mengine nchini na nje ya Kenya ili kufanya utafiti. 

Eastern & Southern Africa Centre of International Parasite Control (ESACIPAC) ilianzishwa huko KEMRI kwa usaidizi wa serikali ya Japani, kupitia JICA chini ya ari ya uzuifu wa vimelea ya ulimwengu. Lengo la ESACIPAC ni kushughulika na kufanikisha masuala ya wafanyikazi ili kutilia nguvu utafiti na taratibu za kuzuia magonjwa yaliyo na vimelea katika sehemu za Afrika mashariki na kusini. Kituo hiki cha ‘Centre for Global Health Research’ (CGHR) kina historia ndefu ya utafiti juu ya malaria kwa kipindi cha miaka 30.Kituo hiki kina vifaa vya hali ya juu.

Sammy M. Njenga ana shahada ya udaktari wa falsafa kutoka Liverpool School of Tropical Medicine, UK.Yeye ni mtafiti mkuu wa sayansi KEMRI na mkurugenzi wa Eastern and Southern Africa Centre of International Parasite Control (ESACIPAC).Utafiti wake unajihusisha na magonjwa yaliyosahaulika katika nchi zenye joto (NTD) yakiwemo magonjwa ya ‘lymphatic filariasis’, kichocho, and ‘soil-transmitted helminthiasis.’

Andrew Githeko ana shahada ya udaktari wa falsafa katika elimu inayohusu vekta na entomolojia-na alisomea Liverpool School of Tropical Medicine.Amekuwa akifanyia kazi ya ugonjwa wa malaria kwa miaka 28 na amekuwa akiangazia ekolojia ya vekta na magonjwa. Kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa akiangazia matokeo ya tabia za nchi na mabadiliko ya mazingira kuhusu malaria katika milima ya Kenya Magharibi. Amethibitisha sehemu ya utafiti katika tabia za nchi na ya afya ya binadamu ambayo imefadhiliwa na NIH, IDRC, USAID, WHO na wengineo. Dr. Githeko amekuwa mwanasayansi wa ‘UN Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC)’ kuanzia mwaka wa 1998 na amehusika katika uandishi wa ripoti zake tatu. Amekuwa mtaalamu na mkaguzi wa ‘Millennium Ecosystem Assessment (MEA).’ Kazi yake ya sasa inahusika na vielelezo vya maambukizi ya malaria, mabadiliko ya kinga kutokana na malaria, jinsi topografia na hydrolojia uathiri epidemolojia ya malaria na jinsi mabadiliko katika matumizi ya arthi yanahusiana na malaria, kuzuia malaria kwa kubadili nyumba na kubadilisha ekolojia ya vinamasi.Anatambua vizuizi na mapengo katika taratibu za kitaifa za kuzuia malaria.

Diana Karanja anakaa CGHR.Utafiti  juu ya kichocho umekuwepo KEMRI tangu mwanzo wake na katika CGHR, ikiongozwa na Dr. Karanja, tangu mwaka wa 1994. Dr. Karanja amefanya kazi juu ya usambazi wa kijiografia juu ya kichocho, elimu ya kingamaradhi, elimu ya uchunguzi wa aina na sababu za ugonjwa na kupeana madawa kwa wingi. Maabara yake yamepokea ufadhili kutoka kwa WHO, NIH, muungano wa CDC, na muungano wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa.

Watafiti wa KEMRI watajihusisha katika kutahini vile mabadiliko ya mazingira husababisha kutokea na kusambaa kwa malaria na kichocho katika Afrika Mashariki (WP3).

Read 34112 times
Translate