Chuo Kikuu cha Trinity cha Dublin

tcd_logo_stacked


Chuo Kikuu cha Trinity cha Dublin,kilianzishwa mwaka wa 1592.Hiki ndicho chuo cha zamani sana nchini Ayalandi.Kwa wakati huu TCD ina wanafunzi zaidi ya 15,700, wafanyikazi 3, 700, na idadi ya wanafunzi 86,000 waliosomea huko, na kwa muda wa 2007-2008 wafanyikazi wake walipewa zaidi ya euro milioni 70 za utafiti. TCD inajulikana kote kwa wanafunzi wake waliohitimu,na pale wamefika ulimwenguni katika utafiti na ufadhili wa masomo, na mchango waliotoa katika nchi ya Ayalandi na ulimwenguni kote.Katika utafiti uliofanywa na THES wa  hivi karibuni (2009) wa vyuo vikuu vya ulimwengu, TDC ilipewa nafasi ya 43 katika vyuo 50 bora ulimwenguni na kupewa nafasi ya 13 katika vyuo 15 bora Ulaya. TDC imegawanywa katika shule 24 za kimasomo zilizosambazwa katika idara tatu (fani, masomo ya sanaa na sayansi za jamii; uhandisi, hisabati na sayansi; na sayansi ya afya). Shule hizi pia huwa na sehemu za utafiti.Isitoshe, TDC pia huwa na; vyuo vya utafiti mbalimbali na ni kiini cha mianzo ya utafiti mbalilmbali, ikiwemo ile ya Trinity International Development Initiative (TIDI). Taasisi mbili zitachangia katika mradi wa Afya Bora ya Baadaye: Chuo cha sayansi ya asilia (idara ya uhandisi, hisabati na sayansi) na kituo cha afya ya ulimwengu (idara ya sayansi ya afya).

Chuo cha sayansi ya asilia hujihusisha na masomo ya botania,jiografia,jiolojia,zuolojia,kituo cha mazingira na kituo cha bioanuia na maendeleo endelevu na ndicho chuo kikubwa zaidi  cha sayansi katika idara ya uhandisi,hisabati na sayansi.Chuo hiki huwa na wafanyikazi 40 (Wanasayansi wa biolojia,wanasayansi wanaojihusisha na vitu visivyokuwa na uhai, wanasayansi wa kijamii), watafiti 20 wa uzamili, wanafunzi 140 wa utafiti na wanafunzi  kama 50 wanaofanya uzamili wa kisayansi na chuo hiki huwa na euro milioni 4 za kila mwaka za utafiti. Wafanyakazi katika chuo hiki hutoa machapisho kadiri ya 150 kila mwaka, mengi yakiwa ni majarida ya hali ya juu ya kisayansi. Sehemu muhimu zaidi za utafiti katika chuo hiki huwa ni mabadiliko katika mazingira (ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi) historia ya mazingira, elimu inayohusu uzalishaji, usambazaji na utumiaji bidhaa pamoja na utandawazi.

David Taylor amekuwa Profesa wa jiografia katika chuo kikuu cha TDC kuanzia Januari 2001. Utafiti wake mkuu unahusu mazingira katika nchi zilizo na joto, na hasa kwa kiasi gani mabadiliko ya mazingira katika Afrika ya Kati na Mashariki yanahusu binadamu na ekolojia. Akiwa alifanya shahada ya udaktari wa falsafa nchini Uganda mwanzoni wa miaka ya 80, David sasa ana zaidi ya miaka 25 ya uzoefu wa kufanya utafiti katika sehemu hizi na zingine zenye joto.Utafiti mwingi umehusu sehemu zenye unyevunyevu.

Laragh Larsen ana shahada ya udaktari wa falsafa katika historia/siasa za jiografia ya miji na kuishi mijini katika nchi za Afrika Mashariki. Amefanya utafiti juu ya jiografia ya binadamu nchini Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. Utafiti wake wa sasa unahusu mabadiliko ya mazingira ya mijini Afrika Mashariki.

Kituo cha afya ya kiulimwengu

Kituo hiki cha afya ya kiulimwengu, TDC, kinajumuisha wafanyakazi 15 na uratibu utafiti na masomo ya waliohitimu shahada ya kwanza katika uwanja wa afya ya kiulimwengu, ikiwa na ratiba za shahada ya udaktari wa falsafa.Kituo hiki hulenga kushughulikia shida za kiafya na mambo yanayopita mipaka ya kitaifa wakiamini kuwa magonjwa ya ulimwengu huwa yanagawanyika na hivyo basi yanafaa kutatuliwa kwa ushirikiano wa pamoja ili kutatuliwa vinavyofaa. Hivyo basi kituo hiki hujihusisha na kutilia nguvu taratibu za kiafya zilizoko kupitia sera na utafiti unaohusiana na taratibu za kiafya.
Read 9777 times
Translate