Taasisi ya Metorolojia na Hydrolojia ya Uswidi (SMHI)

smhisvartjpg


Sveriges Meteorologiska och Hydrologiska Institute (SMHI) ni mojawapo ya idara za kiserikali katika wizara ya kimazingira nchini Uswidi. SMHI hutoa  huduma mbalimbali kwa mashirika mbalimbali kama vile ujumbe kuhusu mazingira kuwezesha mashirika haya katika kutoa uamuzi.Nyanja kubwa zinazolengwa ni pamoja na hali ya hewa na utabiri  wa tabia ya nchi, huduma za viwanda maalumu, ujumuishaji na utathmini, na takwimu. SMHI ina nguvu katika utafiti na maendeleo(R&D),na inatilia nguvu kukuza huduma hizi na kuziendeleza kulingana na vile tabia ya nchi inavyoendea. Utafiti wa tabia ya nchi hujihusisha na sehemu sita za utafiti katika idara za utafiti kikiwemo kituo cha Rossby kinachohusishwa na shughuli za vielelezo vya tabia ya nchi.

Colin Jones ndiye kiongozi katika kituo cha Rossby, akiwa na ujuzi wa zaidi ya miaka 20 katika kukuza vielelezo vya tabia ya nchi. kabla ya kuongoza kituo cha Rossby, alikuwa mkurugenzi wa Canadian Regional Climate Modeling Network na profesa katika Chuo Kikuu cha Quebec, Montreal.Yeye ni mmoja wa viongozi katika WCRP Task-Force na mtaalamu aliyealikwa katika vikao vya WCRP WGCM na WGNE. Ni mmoja wa viongozi wa mradi wa WCRP CORDEX (Coordinated Regional Downscaling Experiment).Yeye pia ni mshiriki wa kikundi cha uelekezaji cha EC-Earth.  Amehusika katika zaidi ya miradi kumi na kuratibu utafiti wa ubia katika nchi na ulimwenguni.Ujuzi wa utafiti wake unajihusisha na uundaji wa vielelezo vya tabia ya nchi.

Patrick Samuelsson ni mwanasayansi katika kituo cha Rossby kilicho SMHI.Yuko na shahada ya udaktari wa falsafa ya maarifa ya tabia ya nchi. Amehusika pia na kufanikisha SURFEX na anajihusisha zaidi na njia na matokeo ya harakati zinazohusiana na mimea, mchanga na maziwa.Alifanya kazi kama kiongozi wa WP katika mradi wa CLIME wa FP5. Hivi sasa amejihusisha na miradi ambayo hutumia RCA katika Ulaya, Akitiki, Afrika na Amerika kusini.

Grigory Nikulin ni mwanasayansi katika kituo cha Rossby. Katika utafiti wake amejishughulisha na kutathmini vielelezo vya tabia ya nchi na kuchunguza mandhari ya nchi katika skeli zote kiulimwengu na sehemu zilizokaribiana. Yuko na ujuzi wa kuchunguza hifadhidata kubwa, akishughulika hasa na takwimu za hali ya juu.Sehemu kubwa ya utafiti wake huangazia jinsi takwimu za hali ya hewa na tabia ya nchi zinavyoweza kugeuka katika siku za usoni.Amehusika pia na kutathmini na uchanganuzi wa tabia ya nchi katika maeneo yanayokaribiana ya Ulaya na Afrika Magharibi (ENSEMBLES).

Katika mradi wa Afya Bora ya Baadaye, SMHI itafanya uigaji wa tabia za nchi ya sehemu zinazokaribiana katika eneo lote la bara la Afrika na kuangazia sehemu inayotafitiwa.Uigaji huu utarejelewa nyuma kwa miaka 50 na kwa siku za usoni kuanzia hivi sasa hadi mwaka wa 2100. Matukio ya siku za usoni yatatumia matukio ya kiulimwengu ya tabia za nchi yatakayotokana na kielelezo cha mradi unaouganisha wa 5 (CMIP5), ukichunguza baadhi ya vielelezo vya tabia za nchi za ulimwengu na gesi zinazoadhiri hali ya hewa.Matokeo yatachunguzwa na yale ambayo hayaeleweki vyema yatatambuliwa na wataalam wa magonjwa watahusishwa. SMHI itafanya kazi kuwasilisha hifadhidata kuhusu tabia ya nchi kwa wataalamu wa magonjwa na kuhusika katika uhusiano kati ya magonjwa na tabia ya nchi kwa wakati huu na jinsi uhusiano huu unatarajiwa kubadiliko katika siku zijazo kama mabadiliko ya mazingara yatazidi kuvuma.
Read 8700 times
Translate