Chuo Kikuu cha Paris Lodron cha Salzburg, Austria (PLUS)

plus_salzburg


Chuo Kikuu cha Paris Lodron cha Salzburg hivi sasa kina zaidi ya wanafunzi 14,000 na takribani ya wafanyakazi 2,700. Kama kiungo kinachoshikanisha utamaduni na elimu, chuo hiki hutumika kama mahali pa kukutana kwa wafanyakazi, wanafunzi na wataalamu katika masomo pamoja na raia wa kawaida. Tangu kianzishwe upya mwaka wa 1962, chuo hiki kimeendelea kupeana masomo na utafiti wa hali ya juu.

Kituo cha Geoinformatics (Z_GIS, www.zgis.at), ni chuo kinachojihusisha na maeneo ya taaluma zaidi ya moja (huwa na wanasayansi 35 wa kiufundi) na kimejitolea kwa dhati katika utafiti unaotumika, shughuli za nje, masomo weledi na mafundisho. Kama wataalamu wa Z_GIS huangazia juu ya matumizi ya GIS, sehemu ya vielelezo, utambuzi wa mbali wa satalaiti, mchanganuo wa michoro, Katagrafi ya dijito, na mawasiliano ya GI.Kwa muda wa miaka ishirini sasa, Z_GIS imepanga kongomano lililoongoza katika nchi zinazozungumza Kijerumani na lilianza miaka mitatu iliyopita na kikao kuhusu ‘Geospatial Crossroads’.Tangu mwaka wa 1998 imejihusisha na shughuli za ‘RTD’ zilizofadhiliwa na Muungano wa Ulaya, ufanisi wa uratibu na miradi ya masomo. Utafiti wa Z_GIS unakuza tekinolojia mpya za maamuzi -huhimili na kuweka mashauri na hivyo basi kuchangia zaidi katika kuangazia, kuelewa, kusimamia mawasiliano, mashauri yanayofaa,na taarifa katika njia iliyowazi.Methodolojia za computer na vifaa hutumika ili  kutathimini mandhari ya nchi  na miji, usimamizi wa maji na mazingira, kuzuia mzozano na migogoro katika kuangazia maendeleo endelevu.Lengo la kituo hiki hasa  ni kuweka pamoja data ya ‘geo-spatial’ na taarifa za kila wakati kutoka kwa mtandao: kituo hiki ni kituo bora cha machanganuo ya michoro. Z_GIS inaendeleza utaratibu wa kuelewa matukio katika anga kwa viwango mbalimbali kwa kulenga utafiti juu ya mazingira na usalama wa binadamu.

Peter Zeil, mtaalamu wa elimu ya fisikia ya dunia,ni msimamizi mkuu wa mradi wa Z_GIS akiwa na zaidi ya miaka 20 ya ustadi barani Ulaya , Afrika, Asia, na  Amerika ya kusini unaohusiana na taarifa za dunia na utambuzi wa mbali kwa ajili ya usimamizi wa raslimali na ujenzi wa mashirika, utaratibu wa ufanisi, kuhamisha teknolojia, uhimili wa maeneo yanayokaribiana na ujenzi wa kunganisha watu. Ana ujuzi mkubwa katika mipango, usimamizi na kutathmini miradi, akiwa amechangia UNESCO baadhi ya tathmini.Yeye ni mmoja wa washiriki wa kikundi mkinaifu cha kuthibitisha cha GMES,na ni mmoja wa wakurugenzi wa Chama cha Afrika cha utambuzi kwa umbali wa mazingira (African Association for Remote Sensing of the Environment (AARSE)).

Stefan Kienberger alipokea shahada yake ya uzamili juu ya sayansi ya mazingira na jiografia kutoka Chuo Kikuu cha Graz, Austria na Chuo Kikuu cha Macquarie, Australia.Utafiti wa shahada yake ya udaktari wa falsafa ulihusu ukadiriaji wa maeneo yanayoweza kukabiliwa na madhara katika taarafa na maeneo maalum nchini Mozambique.Utafiti wake ulihusisha maeneo yanayokumbwa na hatari za aina mbalimbali na kuunganisha methodolojia za sayansi ya GI na ile ya utambuzi kwa umbali. Pamoja na hayo, amejumuika katika miradi ya kujenga uwezo (GIS) na ana kazi na ujuzi wa utafiti katika Afrika Kusini, Asia, na sehemu zilizotahiniwa barani Ulaya.

Watafiti wa PLUS wanajihusisha na kuunganisha data mbalimbali katika sehemu za mambo fulani. PLUS huongoza kazi ya 2.3 ili kutoa habari mbalimbali za sehemu za ardhi/ matumizi ya taarifa na kupeana data iliyotathmiwa ya maandhari. Mchango mwingine mkubwa ni namna utafiti utafanyika katika sehemu zinazokumbwa na hatari WP4 (4.1) na pia kuweza kutambua magonjwa yanayohatarisha na yanayoweza kudhuru (4.8) kama kipengele cha ufanisi katika kuwezesha kuweko kwa vifaa vya kutoa usaidizi katika WP5. Wafanyakazi wa PLUS (pamoja na CGIS-NUR) watasimamia mojawapo ya shahada za udaktari wa falsafa zinazothaminiwa na Mradi wa Afya Bora ya Baadaye.
Read 10349 times
Translate