Shughuli za Mradi wa Afya Bora ya Baadaye zimetawanywa katika miaka miine, mradi ukilenga kushughulikia magonjwa matatu katika Afrika Mashariki.Sababu ya kuchagua Afrika Mashariki kama eneo la utafiti kunadhibitisha kwamba maeneo yote katika jamii-ikiwemo mashirika ya kimataifa kama vile Muungano wa Afrika Mashariki (EAC) na Muungano wa Ulaya( EU)- yako tayari kuwezesha kutekeleza matokeo ya utafiti na kuongezea kuelewa utafiti wa kisayansi kwa minajili ya kupunguza athari za mazingira,pamoja na mabadiliko katika tabia ya nchi.
Mradi wa Afya Bora ya baadaye umegawanywa katika kazi saba (WP)zinazohusiana ili kutimiza malengo yake na kutatua maswali yatakayotokana na utafiti.Kazi hizi zitatimiza malengo haya kwa:
1)Kutoa usimamizi unaofaa na kukagua mradi huu na miradi mingine inayohusiana na mradi wa Afya Bora ya Baadaye ili kuhakikisha kwamba yaliyopangwa yataweza kutekelezwa katika viwango vya mitaa,taifa na mikoa( WP1)
2) Kuhakikisha kwamba kuna faida kubwa inayotokana na mradi huu kufanya kazi pamoja na miradi mingine barani Afrika na maeneo ya mbali ( WP7)
3)Kuunda sera muhimu zinazoweza kuigwa na kutumiwa ili kutabiri uhusiano katika mazingira na magonjwa yale matatu yanayosababishwa na maji (VBDs) uhusiano huu ukiliganishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo na misimu mbalimbali na jinsi hali ya siku za baadaye itakavyokuwa katika jamii na uchumi,matumizi ya ardhi(hasa ukulima wa maeneo makubwa,kilimo shadidi,ukuzaji wa miji na makazi yasiyokuwa ya kudumu(WPs 2,3,4)
4) Kukagua kwa maakini,na kama ni muhimu, kuongezea mathibitisho yalioko katika eneo linalofanyiwa utafiti yanayoelezea uhusiano katika mazingira( pamoja na tabia ya nchi) na afya na kutoa mawaidha yatakayosulihisha kukusanya data,kuuhifadhi na kuichambua(WPs 1,2,3),
5) Kuunganisha pamoja uigaji ulioelezewa hapo awali(3) na kuelewa jinsi magonjwa yale matatu yanavyozuka-pamoja na kuelewa uhusiano wa siku zilizopita katika mabadiliko ya mazingira na hali ya kijamii na kiuchumi na uzukaji wa magonjwa haya matatu-kubashiri uwezekano wa kuzuka na kuenea kwa magonjwa haya na kuboresha jinsi ya kugundua uwezekano wa magonjwa haya kuzuka tena katika siku za usoni (WPs 3,4).
6) Kuongezea uwezo wa huduma za afya na afya ya mifugo mitaani, kwa taifa na mikoani ili kuweza kukabiliana na mabadiliko katika usambazaji na uzukaji wa magonjwa yale matatu yanayotokana na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi,matumizi ya ardhi,na hali katika jamii na uchumi kwa kutumia vifaa vya kutoa uamuzi (WP5),
7)Kuhakikisha kuwa matokeo ya utafiti huu yameenezwa kati ya washika dau,watunga sera,na jumuia ya wanasayansi ulimwenguni.Isitoshe,matokeo haya,ikiwemo vifaa vya kusaidia kutoa uamuzi,yatatolewa kwa wakaazi wa maenoe ambayo hukumbwa na mlipuko wa magonjwa pande zingine za Afrika(ambazo hazishughulikiwi na mradi huu) na,kama uhusiano utakuwepo,maenoe haya yatachukuliwa kama oya la mapema na Ulaya na utaratibi wa kupunguza magonjwa haya utawekwa.
Kazi mbalimbali katika mradi huu zimeundwa kuhakikisha kwamba mradi utasimamiwa kama ipasavyo,na kwamba yaliyokusudiwa kutolewa na kutawanywa yatafanywa hivyo katika wakati na bajeti ifaayo. Ubia wa mradi wa Afya Bora ya Baadaye unajihusisha na mabadiliko ya mazingira,afya ya binadamu na wanyama, sayansi ya jamii na siasa pamoja na utaalamu wa kukumbana na mabadiliko katika tabia ya nchi katika vyuo 15 barani Afrika na Ulaya.Kazi nyingi za mradi huu zitahudumiwa kwa pamoja na viongozi wawili,mmoja akiwemo kutoka Afrika,na mwingine Ulaya.