MYM na maoni

Rate this item
(4 votes)

1. Mradi huu hufadhiliwa na nani?

Mradi huu wa Afya Bora ya Baadaye umepokea ufadhili wa milioni €3.38 kupitia kwa mradi wa 7th framework programme (FP7), ambacho ni kifaa cha Muungano wa Ulaya kinachofadhili utafiti Ulaya. FP7 iliundwa kusaidia maendeleo ya Ulaya kuweza kushindana,katika ajira, na ubora wa maisha. Mradi wa FP7 ulianzishwa mwaka wa 2007 na utaendelea hadi 2013. Bonyeza hapa kwa habari zaidi juu ya FP7.

2. Ni nini hasa motisha wa Mradi wa Afya Bora ya Baadaye?

Mlipuko wa magonjwa ya vekta yanayosababishwa na maji, kama vile malaria, yanauhusiano changamani na mazingira. Hali ya mazingira inavyoendelea kubadilika, kama vile kupitia ubadilikaji wa tabia ya nchi na matumizi ya ardhi, ndivyo basi kuenea kwa magonjwa kunaweza kubadilika. Hata kama wale wote wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na mlipuko wa magonjwa haya wako hatarini, wale watakaoathiriwa zaidi ni waliotengwa katika jamii. Mradi wa Afya Bora ya Baadaye unuia kupunguza mashaka haya kwa kuboresha uwezo wa kutabiri na kuelezea kiasi na ukali wa mlipuko wa magonjwa wa siku zijazo katika hali tofauti za mabadiliko ya mazingira.

3. Ni kwa nini magonjwa haya matatu yenye uhusiano na maji na vekta yalichaguliwa?

Magonjwa mawili kati ya matatu yanayoshughulikiwa na mradi huu (malaria na homa ya bonde la ufa) yanasababishwa na vekta. Ugonjwa wa tatu (kichocho) husababishwa na konokono. Lakini kwa urahisi magonjwa yote matatu yanajulikana kama VBDs (Vector-borne diseases)katika mradi huu na viumbehai vinavyoeneza viini hivi hujulikana kama vekta. Magonjwa haya matatu yalichaguliwa kutokana na uhusiano ulioka kati ya vekta na vimelea na kutokana na maandishi mbalimbali yaliyochapishwa kuhusu uhusiano ulioko kati ya mabadiliko ya mazingira na athari za kiafya kwa binadamu ,wanyama na uchumi zinazotokana na mabadiliko haya na pia kwa sababu ya ushirikiano wa karibu uliopo kati ya magonjwa haya na watafiti wa ubia wa Afya Bora ya Baadaye. Isitoshe, magonjwa haya matatu uambukizwa kwa njia tatu tofauti ijapo kuwa magonjwa yote matatu yataathariwa na mabadiliko ya hali ya mazingira, tabia ya binadamu ikiwa muhimu sana katika kuamua matokeo halisi.

4. Kwa nini eneo hili la Afrika limeangaziwa?

Athari na kutawanyika kwa magonjwa ya vekta yanayohusiana na maji (VBDs) zina vuka mipaka. Sababu ya kuchagua Afrika Mashariki kama eneo la utafiti kunadhibitisha kwamba maeneo yote katika jamii-ikiwemo mashirika ya kimataifa kama vile Muungano wa Afrika Mashariki (EAC) na Muungano wa Ulaya( EU)- yako tayari kuwezesha kutekeleza matokeo ya utafiti na kuongezea kuelewa utafiti wa kisayansi kwa minajili ya kupunguza athari za mazingira, pamoja na mabadiliko katika tabia ya nchi.Baadhi ya maeneo yaliyoinuka(kutoka usawa wa bahari) na yaliyoko mbali au karibu na ikweta yaliyo na uhusiano na mabadiliko ya mazingira, yakiwemo maeneo makubwa ya milimani na ya nyanda za chini za pwani, zikiwemo sehemu zenye hali ya unyevunyevu inayotofautiana, zenye unyevunyevu mwingi na zile zenye ukavu, zinashughulikiwa katika eneo la utafiti huu. Tena, maeneo makubwa ya maji baridi pamoja na sehemu kubwa za unevunyevu,ambazo hivi sasa zinatumiwa kukuza vyakula, pia zinashughulikiwa na mradi huu.Tofauti hii ya mazingira inalingana na tofauti ya watu wenye lugha,dini, utamaduni na makaazi mbalimbali, pamoja na mgawanyo wa watu na shuguli za uchumi usiokuwa na usawa, sehemu za milimani zikiwa na idadi ya watu wengi zaidi.Hata kama mradi wa Afya Bora ya Baadaye unaangazia Afrika Mashariki kama eneo lake ya utafiti, mbinu iliyochukuliwa na matokeo ya utafiti yanatarajiwa kuweza kutumika sehemu zinginezo za Afrika na Ulaya.

5. Mradi wa Afya Bora ya Baadaye unatarajia kuwa na matokeo gani?

Kwa jumla,mipango ya kazi ya mradi hunuia kuunda sera muhimu zinazoweza kuigwa na kutumiwa ili kutabiri uusiano wa mazingira na magonjwa yale matatu yanayosababishwa na maji (VBDs) uhusiano huu ukiliganishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi katika maeneo na misimu mbalimbali na jinsi hali ya siku za baadaye itakavyokuwa katika jamii na uchumi, na matumizi ya ardhi. Uigaji huu utatumiwa kuelewa jinsi magonjwa yale matatu yanavyozuka-pamoja na kuelewa uhusiano wa siku zilizopita katika mabadiliko ya mazingira na hali ya kijamii na kiuchumi na uzukaji wa magonjwa haya matatu-kubashiri uwezekano wa kuzuka na kuenea kwa magonjwa haya. Matokeo haya yatatumiwa kuboresha jinsi ya kugundua uwezekano wa magonjwa haya kuzuka katika siku za usoni na pia kama msingi wa kuchunguza vyema zaidi mlipuko wa magonjwa na kama mfumo wa mapema wa kutoa onyo dhidi ya magonjwa haya. Mradi wa Afya Bora ya Baadaye pia hulenga Kuongezea uwezo wa huduma za afya na afya ya mifugo mitaani, kwa taifa na mikoani ili kuweza kukabiliana na mabadiliko katika usambazaji na uzukaji wa magonjwa yale matatu yanayotokana na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi, matumizi ya ardhi, hali katika jamii na uchumi. Lengo hili litatimizwa kwa kuboresha jinsi ya kugundua uwezekano wa magonjwa haya kuzuka na kuweko kwa mfumo wa mapema wa kutoa onyo dhidi ya magonjwa haya kwa njia ya kutumia vifaa vya kutoa uamuzi.Matokeo yatatolewa kama mradi utakavyokuwa unaendelea.

6. Mradi utafanya kazi katika kiwango gani ili kuelewa uwezekano wa magonjwa haya kuzuka na ni wapi magonjwa haya yanaweza kuzuka?

Mradi wa Afya Bora ya Baadaye unuia kufanya kazi katika viwango viwili. Katika kiwango cha kwanza, uwezekano wa kuzuka kwa magonjwa unakaguliwa katika sehemu maalum za nchi. Nchi za Afrika mashariki zinazotumiwa kwa utafiti huu ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi. Ubia wa Afya Bora ya Baadaye una kusudia kuonyesha sehemu katika nchi hizi ambazo zinawezwa kukabiliwa na magonjwa yale matatu ya vekta. Uwezekano wa kuonyesha sehemu hizi zenye mashaka utalingana na hifadhidata itakayotolewa ya tabia ya nchi pamoja na data itakayoonyesha ubadilikaji katika hali ya ki-jamii na ki-uchumi. Lengo maaluum haswa ni kuonyesha sehemu mbalimbali za nchi ambazo ziko hatarini na ambazo zinaweza kukabiliwa na magonjwa haya.

Kiwango cha pili kinahusu kukagua seheme zenye mashaka mitaani. Sehemu zifwatazo zimechaguliwa kutafitia magonjwa yale matatu ya vekta katika kiwango cha mitaani na mikoani.

  • Sehemu iliopendekezwa kutafitiwa malaria na kichocho: ziwa Burera, Rwanda
  • Sehemu iliyopendekezwa kutafitiwa kichocho; wilaya ya Buliisa,ziwa Albert, Uganda
  • Sehemu iliyopendekezwa kutafitiwa homa ya bonde la ufa na malaria;Ijara, Kenya

  • 7. Nitawezaje kujijulisha zaidi juu ya shughuli za mradi huu?

Shughuli za mradi huu zitatangazwa katika tovuti hii,kwa hivyo tafadhali angalia tovuti kwa habari zaidi. Pia washiriki-ubia watakusanya pamoja habari na kuzitawanya katika toleo mbalimbali na majarida. Lakini, jinsi ya kuarifiwa wakati wowote (na kufaidika kutokana na shughuli zetu) ni kuwasiliana na washiriki wetu katika nchi yako au kutuma swali lako kwa njia ya barua pepe hapa.

8. Washika dau na watakaofaidika kutokana na mradi huu ni nani?

Ili kuweza kutawanya habari ya mradi wa Afya Bora ya Baadaye kama ipasavyo, ni muhimu kutambua wale watakaofaidika kutokana na maarifa ya mradi huu. Lengo moja muhimu la mradi huu ni kujenga hifadhidata ya washika dau na watakaofaidika kutokana na shughuli za mradi wa Afya Bora ya Baadaye. Mfano ya washika dau na watakaofaidika ni;

  • Jumuia ya wanasayansi ulimwenguni wakiangazia afya (ulimwenguni) na magonjwa yaliyosahaulika katika nchi zenye joto
  • Watunga sera na wanaotoa mashauri (serekali za mataifa,Ulaya na Ulimwengu) ya afya
  • Wanainchi kwa jumla

Maoni
Mradi wa Afya Bora ya Baadaye unakaribisha maoni yanayohusiana na shughuli zake. Tafadhali bonyeza hapa kutoa maoni yako.

Read 10393 times
Translate