Muhtasari

Mradi wa Afya Bora ya Baadaye kwa Muhtasari

 


 

Mada: Afya, mabadiliko ya kimazingira na; uwezo wa kurekebisha; mitindo ya magonjwa; kutathmini na kutazamia hatari za siku za baadaye zinazohusiana na magonjwa yasababishwayo na maji ‘vector-borne diseases’ yanayohatarisha nchi za Afrika Mashariki.

Ratiba: Shirika la FP7, Mazingira (ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi)

Vifaa: Mradi wa pamoja (miradi midogo au ya wastani inayoangazia utafiti)

Bajeti: €4,194,963

Mchango wa Muungano wa Ulaya: €3,377,998

Muda: Januari 2011- Disemba 2014

Mratibu: Trinity College Dublin, Ireland

Ubia: Washiriki ni 16 ambao 8 huwa Afrika, 7 huwa Ulaya na 1 ya Kusini-mashariki mwa Asia-msingi


Fauka na  kushughulikia mahitaji ya Muungano wa Ulaya ya 7th Framework,shughuli ndogo ya 6.1.2 ya kimazingira na afya , Sehemu 6.1.2.1 uathiri wa kiafya unaosababishwa na mabadiliko  ya kimazingira, ENV.2010.1.2.1-1 (Athari za mabadiliko ya mazingira katika matukio na usambazaji wa magonjwa yasababishwayo na maji barani Afrika),Mradi wa Afya Bora ya Baadaye hulenga kujihusisha moja kwa moja na mambo yaliyoangaziwa katika mkutano wa Afya ya Dunia (WHA) 2008 pamoja na kujishugulisha na upungufu wa maarifa uliotambuliwa na Shirika La Afya Duniani(WHO)( Utafiti wa kiulimwengu juu ya  kulinda afya  dhidi ya mabadilko ya hali ya hewa) 2009.

Malengo ya utafiti ulioazimiwa yanaweza kuundwa upya katika baadhi ya maswali ambayo utafiti wa Mradi wa Afya ya Bora ya Baadaye utashughulikia, hasa madhumuni ya ENV.2010.1.2.1-1:

- Ni hali gani katika mazingira husababisha usambazaji na shughuli za vekta au wanyama wanaosambaza magonjwa katika Afrika Mashariki?

- Ni kwa kiasi gani kuzuka kwa haya magonjwa matatu kunadhihirisha hali ya kijamii na kiuchumi, uhamaji, aina mbalimbali za makaazi na mambo ambayo yanaleta migogoro?

- Ni kwa kiasi gani hali hii hivi vinatofautiana na yaliyothibitishwa hapo awali na kumekwa na athari gani za magonjwa kutokana na tofauti hizi?

- Ni kwa kiwango gani ueneaji hasili wa usambazaji na kuzuka kwa magonjwa yale matatu yaliyolengwa unaweza kulinganishwa na uwezekano wa kuenea kwa magonjwa haya, na ni mambo gani hasa yanaweza kusababisha tofauti hizi?

  • - Usambazaji na uzukaji wa magonjwa haya matatu unaweza kutofautiana vipi kulingana na mambo ya kimazingira yaliyokubalika ulimwenguni?

- Ni vipi uwezekano wa mkurupuko na usambazaji wa magonjwa miongoni mwa jamii ambazo zimechanganyika huweza kusababisha mgongano wa magonjwa?

  • - Ni vizuizi vipi vinavyopinga uwezo wa huduma za kiafya na matibabu ya mifugo kuweza kuitikia maonyo yanayohatarisha uzukaji wa magonjwa, na vizuizi hivi vinaweza kutatuliwa kwa njia gani?

- Mabadiliko yaliyotabiriwa ya usambazaji na uzukaji wa magonjwa haya matatu yataathiri vipi sehemu nyingine za Afrika na huko Ulaya.

Mradi huu wa Afya Bora ya Baadaye unashughulikia Afrika Mashariki kama sehemu yake ya utafiti na hujihusisha na nyanja mbalimbali za kiafya, mazingira, jamii na kiuchumi na pia kuonyesha mitindo ya magonjwa ukifanya kazi pamoja na wataalamu wa tabia ya nchi na idara za kiserikali.Ili kuweza kufikia malengo haya, Mradi wa Afya Bora ya Baadaye, utawajumuisha watakaofaidika kutokana na mradi huu pamoja na washika dau na kuleta pamoja utafiti wa uwanja, maabara na wa maktaba.


Case Study Area

Read 14029 times
Translate