WP1: Mradi utakavyosimamiwa
Uratibu na usimamizi wa mradi wa Afya bora ya baadaye hufanyika kupitia kwa WP1, ukiongozwa na AquaTT (Ayalandi), ambao hushughulika na usimamizi wa mradi wa Muungano wa Ulaya na pia kushikilia mratibu wa mradi katika shughuli za kila siku..Mawaidha kuhusu utaratibu unaofuatwa katika kukusanya, kuunganisha na kusimamia data za mradi pia hupeanwa kupitia WP, pia mambo yanayohatarisha, kuhakikisha ubora wa mradi na mipango ya kutathimini.
Bonyeza menyu ilioko upande wa kulia kwa maelezo zaidi
WP2: Maelezo kuhusu magonjwa na kutengenezwa kwa hifadhidata
WP2 uongozwa kwa pamoja na TCD (Ayalandi), ILRI (Kenya), NUR (Rwanda) na ICTP (Italia).Mradi huu wa WP,mkubwa zaidi ukiangalia watu wanaojihusisha kila mwezi,hulenga kuweka pamoja mradi wa hifadhidata inayojihusisha na ujumbe unaohusiana na mkurupuko wa magonjwa matatu yanayolengwa katika sehemu inayofanyiwa utafiti na ujumbe kutolewa kutoka asili za kimsingi na kisekondari.Ujumbe huu huhusisha data ya kihistoria ,kijamii na kiuchumi,uhamaji, makazi na migogoro; vilevile data ya sayansi ya ulimwengu, tabia ya nchi, ukiwemo ujumbe kuhusu uhusiano kati ya magonjwa na mazingira. Hifathidata ya mradi huu itawekwa kwenye tovuti na kuwa tayari kwa washikadau wote wanaojihusisha na utafiti huu.
Bonyeza menyu ilioko upande wa kulia kwa maelezo zaidi
WP3: Uhusiano wa mazingira na usambazaji wa magonjwa pamoja na kuonyesha mitindo
Ikiwa imeongozwa na TRAC Plus (Rwanda), KEMRI (Kenya) na UDUR (UK), WP3 inatarajiwa kufanya utafiti wa uwanjani kutathimini data iliyokusanywa kama mojawapo ya hii WP, na WP 2 na ya 4, ili kuwezesha kuelezea wazi vipengele viliopo katika mitindo ya magonjwa. Mitindo hii, ikiwa ni pamoja na vielelezo vya kihesabu kuhusu maambukizo ya magonjwa ya malaria, homa ya bonde la ufa na kichocho, itafanikishwa na kuenezwa katika WP3.Yatakayotokana na vielelezo hivi yatawekwa kwa WP4 na kutumiwa ili kubuni utaratibu utakaowezesha kugundua magonjwa yanayohatarisha kwa sasa na hali ya baadaye ya anga pamoja na mitindo ya kijamii na kiuchumi.
Bonyeza menyu ilioko upande wa kulia kwa maelezo zaidi
WP4:Hatari za magonjwa na utaratibu wa kugundua magonjwa
ILRI (Kenya), NUR (Rwanda), PLUS (Austria) and SMHI (Sweden) wakijumuika na WP4,hufanyia kazi kati ya WPs2 ( inayoshughlikia magonjwa ya zamani), 3(miundo inayoelezea mitindo ya magonjwa) na 5 (taratibu za uamuzi na egemezo ). Katika WP4 hifadhidata zinazorejelewa kuhusu kinachosababisha magonjwa ya zamani na matukio ya magonjwa haya (zilizokusanyika katika WP2), pamoja na ufahamu na vielelezo vya mitindo ya magonjwa matatu yanoyolengwa na mradi huu(WP3), yatatumika kutoa makadirio kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa magonjwa ya hatari ya zamani na ya sasa na athari zitakazotokana na maradhi hayo.Mvurumisho huu utatilia maanani mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi,athari za hiadrologia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, mabadiliko katika hali ya kijamii na kiuchumi na mabadiliko katika matumizi ya ardhi.Makadirio haya yatafaidi WP5 kwa kupeana vifaa vya kutegemeza na vya kutoa uamuzi na pia maelekezo kuhusu sehemu muhimu sana ambapo utaratibu huu unahitajika.Kulingana na mpangilio wa utafiti, WP4 itajihusisha na mradi huu kupitia viwango viwili: kulenga maeneo maalumu katika nchi tano za Afrika Mashariki zitakazowezesha kudhiinisha sehemu ambazo hukumbwa na hatari za magonjwa haya, na maeneo ya mitaani ambapo mikakati halisi ya marekebisho itajaribiwa.
Bonyeza menyu ilioko upande wa kulia kwa maelezo zaidi
WP5: Ulinganisho na kupeana vifaa vya kusaidia kutoa uamuzi
WP5, ikiongozwa na SEI (Tanzania and Kenya) na ikiitikia ule ushirika wa washika dau, wanaofanya maamuzi na matokeo ya WPs 4(ukisiaji wa hatari na uwezo wa kukabiliwa na maradhi, pamoja na maathiri yanayotokana na maradhi haya) na 6 (habari za washika dau), itatambua na kueneza mikakati halisi ya marekebisho katika mabadiliko ya mazingara na kutumia vifaa vya kusaidia kutoa uamuzi ili kutoa ulinganisho katika maeneo yanayoangaziwa. Isitoshe, mradi wa WP utajihusisha na kuweka warsha ambazo wanaofanya maamuzi watarejelea matokeo ya miradi na pia kuendeleza vifaa vya kutoa uamuzi kuhusu ugonjwa wa homa ya bonde la ufa, vilivyotengenezwa na washika dau kufuatia mkurupuko wa ugonjwa huu hivi karibuni nchini Kenya.Jambo mpya katika WP hii ni kwamba itatumia sampuli ya hapo awali ya ‘Adaptation Decision Explorer’ (ADx)’ ambayo huchanganya vifaa vya kusaidia kutoa uamuzi kwa pamoja.
Bonyeza menyu ilioka upande wa kulia kwa maelezo zaidi
WP6:Kugawanya maarifa na mafunzo kwa washika dau ili kuwashirikisha katika mradi na kuwaongezea uwezo.
WP6,ikiongozwa na TCD (Ayalandi),hujihusisha kwa kuwashirikisha washika dau katika utafiti, kutawanya matokeo ya utafiti, na kujijumuisha katika mafunzo ya shahada ya uzamili kwa njia ya utafiti unaodhaminiwa kupitia kwa Mradi wa Afya Bora ya Baadaye.Jambo la muhimu ni kuweza kubadilishana maarifa na mawazo na washika dau katika warsha mbalimbali, kustawisha ustadi ulioko, na kuendeleza uhusiano wa kiutafiti utakaodumu miongoni mwa washika dau.Kutawanywa kwa matokeo ya utafiti kutafanyika katika kumbi mbalimbali,ikiwemo mikutano miwili ya kimataifa itakayoandaliwa itakapokaribia mwisho wa utafiti wa mradi huu.Kiini cha ukumbi wa kwanza kitakuwa mabadiliko ya kimazingira na afya kwa ajili ya kongomano la 8 la Ulaya linaloshughulikia dawa za kutoka nchi zenye joto na afya ya ulimwengu (ECTMIH).Ukumbi wa pili utakuwa warsha ya Afrika na Ulaya, itakayosimamiwa na NUR,Rwanda, ikiaangazia kuunganisha swala la mabadiliko ya tabia ya nchi na wataalamu wa afya (katika kurekebisha na sera), hasa kuhusu magonjwa yale matatu yanayolengwa na Mradi wa Afya Bora ya Baadaye,huku ikizingatia kukagua methodolojia ya jumla iliyochukuliwa na matokeo ya utafiti kutoka sehemu zingine( kwa mfano pande zingine za Afrika na baadhi ya sehemu za Ulaya) ambazo huchukuliwa kama sehemu zenye mashaka. Magonjwa mengine ya kuangaziwa ni ‘Blue tongue’ na ‘West Nile Virus.’
Bonyeza menyu ilioko upande wa kulia kwa maelezo zaidi
WP7: Kuongezea nguvu katika utafiti na matumizi ya utafiti
WP7,ikiongozwa na Aquatt (Ayalandi),itakuza nguvu mpya katika mradi,na kufanya kazi kwa pamoja na miradi ya utafiti inayoshughulikia tabia ya nchi na afya inayodhaminiwa na Muungano wa Ulaya, FP na washika dau wengine wasiokuwa wa Muungano wa Ulaya, ikiwemo watafiti wa kiulimwengu na walio majirani. WP itatoa usimamizi, na kutathmini matokeo ya mradi, kuonyesha mwongozo utakaofuatwa baadaye na kuwa na mazoea ya hali ya juu yanayoongozwa na maadili. WP itatenda kazi kupitia penali ya wataalamu wa ukaguzi, watakaoongozwa na mtaalamu mwenye ujuzi wa mambo yanayohusu mradi huu wakiwa pamoja na washiriki wengine wasiokuwa wa mradi wa Afya Bora ya Baadaye (kati ya hawa, wawili, watakuwa waakilishi kutoka ECDC na kutoka EAC).Penali ya wataalamu hawa pia itawahusisha washiriki watatu kutoka kwa mradi wa Afya Bora ya Baadaye, mmoja akiwa anakaa Afrika na mwingine akiwa anakaa Ulaya. Sababu ya kuwashirikisha hawa watatu katika usimamizi wa mradi huu ni kuhakikisha kuwa kuna mfululizo kati ya makundi haya mawili. Pia ili kuwe na usawa wa kijinsia.
Bonyeza menyu ilioko upande wa kulia kwa maelezo zaidi