Viungo Muhimu

Miradi inayofaa


Kuelezea kiasi cha athari zinazotokana na hali ya hewa na tabia ya nchi katika nchi zinazoendelea

Watatu kati ya washiriki wa Afya Bora ya Baadaye (ICTP, ILRI, UNILIV) ni washiriki wa mradi mpya wa Muungano wa Ulaya QWeCI ambao watachunguza kimwezi na kimsimu uwezekano wa kuzuka kwa malaria na homa ya bonde la ufa katika nchi tatu za Afrika zilizolengwa na mradi wa Afya Bora ya Baadaye.Ukiwa utaanza mwaka wa 2010, QWeCI, mradi uliofadhiliwa na Muungano wa Ulaya FP7, utaratibu mkusanyiko wa data kuhusu magonjwa ya mifugo na binadamu hasa malaria na homa ya bonde la ufa nchini Ghana, Malawi na Senegali.Uwezo wa mradi wa Afya Bora ya Baadaye kuelezea mitindo ya magonjwa haya utanufaika kupitia uhusiano wa karibu na QWeCI. QWeCl inalenga kutumia takwimu na mitindo ya kuonyesha shughuli za vekta ili kuweza kuelezea hatari zinazowezakutokana na magonjwa ya malaria na homa ya bonde la ufa katika muda wa kimwezi hadi kimsimu na zaidi, na kuchunguza njia mwafaka za kuzitawanya habari hizi kwa watakaozitumia.


EDENext: Biologia and uzuifu wa magonjwa ya kuambukiza yanayoenezwa na vekta.

EDENext ni mradi wa utafiti unaoleta pamoja makundi 46 ya kimataifa yanayojihusisha na uchunguzi wa biolojia, ekolojia na epidemolojia ya sehemu za magonjwa yaenezwayo na vekta,  kuzuka na kusambaa na uundaji wa vifaa vipya vya kuyazuia.

EDENext huongezea mawazo, methodolojia, vifaa na matokeo ya miradi ya awali ya EDEN (Emerging diseases in a changing European environment). EDENext inatumia njia ile ile ya jumla ya kuweza kuleta ufanisi kupitia vifaa vya hali ya juu kuboresha uzuiaji, uangaliaji na uthibitishaji kuhusu vekta na magonjwa yanayosababishwa na vekta. Hata kama EDEN iliangazia matokeo ya mabadiliko ya mazingira kutokana na kuzuka kwa magonjwa yanayosababishwa na vekta ,EDENext nayo inatafuta kuelezea na kuonyesha jinsi magonjwa haya yanaanza, na kuenea na itatathmini njia za uzuiaji wa kuenea kwa magonjwa haya.

EDENext huangazia makundi ya vekta: kupe, panya, wadudu mbu, Culicoides, na nzi wa mchangani.Miradi hii ya vikundi imehimiliwa na muungano wa timu inayojihusisha na Afya ya uuma, vielelezo na usimamizi wa data.

Viungo vingine ambavyo vinaweza kukuvutia

EDENext Data Portal (kiungo hiki kitaanzishwa msimu huu wa kiangazi).Kabla ya wakati huo kiungo hiki kitakurejesha kwa kiungo cha zamani cha EDEN Data Site.

Kifaa cha kutafuta machapisho ya EDEN- zaidi ya nakala 250 kuhusu magonjwa yanayosababishwa na vekta au yanayohusiana nayo zimepeanwa ili zichapishwe.


Kuzuia Kuenea kwa Ugonjwa wa Kichocho

CONTRAST ni muungano unaoleta pamoja ujuzi na utaalamu ili kuzalisha maarifa mapya juu ya biolojia, mazingira na mambo ya kijamii na kiuchumi yanayohusiana na ugonjwa wa kichocho barani Afrika.Mradi huu utaingiana na kampeni zinazoendelea za kemotherapi ulio na msingi wa dawa ya ‘praziquantel’ na itatoa matokeo yatakayodumu juu ya ugonjwa huu.Mradi huu utajihusisha kujua namna ya kuelewa jinsi kichocho uenea, ili kulenga na kuweza kujua namna nzuri ya kutumia raslimali ili kuuzuia ugonjwa huu.


Kuungana Pamoja ili Kuzuia Magonjwa Yanayoenezwa na Vekta

ICONZ hulenga kuboresha afya ya binadamu na uzalishaji wa mifugo katika nchi zinazoendelea kupitia kuzuia magonjwa ya kuambukiza kati ya wanyama, ikiwa na uvumbuzi wa kisayansi na kuhusisha raia. ICONZ huunganisha wataalamu kutoka nchi 21 za Ulaya na mashirika mengine barani Afrika wakiungana pamoja kufanikisha mikakati inayofaa ya kuzuia magonjwa ya kuambukiza kati ya wanyama na binadamu.Ili kuweza kuzuia magonjwa haya katika wanyama uvumbuzi wa kisayansi utahitajika ili kutambua (na kama ni lazima) kukuza vifaa vya uchunguzi wa magonjwa, na kuelezea kiasi cha matatizo yanayodhuru afya na jinsi ya kuyazuia. Kuhusisha raia na washika dau katika viwango vyote utahitajika ili kuhakikisha kuwa mikakati inafaa wale watakofaidika katika jamii zilizoathiriwa na kwamba mikakati hii inakubaliwa katika sera zilizotungwa na nchi zilizoathiriwa.


Kuongezea wajibu wa sehemu za unyevunyevu katika usimamizi wa maji yaliyoshikamana  katika Muungano wa Ulaya, Afrika na Amerika kusini ili kuhimili  miradi ya maji ya Muungano wa Ulaya

Madhumuni ya mradi huu wa WETwin ni kuongezea wajibu wa sehemu za unyevunyevu katika usimamizi wa maji yaliyoshikamana,na lengo la kuboresha huduma za jamuia na kuhifadhi ikolojia. Mradi utajumuika na uchunguzi kifani wa sehemu za unyevunyevu kutoka ulaya, Afrika na Amerika kusini. Suluhisho kuhusu jinsi maeneo haya ya unyevunyevu yatasimamiwa utatafutwa ili mathumuni yaliotajwa  hapo awali yaweze kufikiwa. Maarifa na uzoefu utakaotokana na uchunguzi kifani yatafupishwa katika  mwongozo wa kijumla ili kuwezesha mradi kutimiza lengo lake katika kiwango cha ulimwengu.Mradi pia unakusudia kuunga mkono mabadilishano ya ujuzi wa kimataifa kuhusu usimamizi wa sehemu za unyevunyevu.Kushiriki kwa washika dau,kuongezea  na kubadilishana maarifa kutaungwa mkono na baadhi ya hafla za washika dau zitakazofanyika.


Upimaji wa hali ya hewa Afrika katila skeli ya kilomita chache: vifaa  na mikakati ya kusimamia  rasilimali

AFROMAISON hulenga kupendekeza mikakati ya  kuwezesha uhusiano katika  usimamizi wa raslimali ili kuwezesha kukabiliana na hali inayotokana na mabadiliko katika tabia ya nchi.Bara la Afrika huonekana kama eneo lenye kuadhirika kwa urahisi kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.Jambo hili linaweza kusababisha ukosefu mkubwa wa maji na madhara mengine kwa ajili ya maafa ya asilia.Inatarajiwa kuwa mabadiliko katika tabia ya nchi yatazidi juhudi zilizoko kwa sasa za kukomesha umaskini. AFROMAISON itapendekeza utatuzi endelevu katika usimamizi na mikakati ya  sera za rasilimali (maji) kwa jumuia na wanaoshikilia mamlaka ,ili kuwasaidia kukabiliana na mabadiliko katika tabia ya nchi.


Kujenga unyumbukaji  baina ya Jumuia ya Ulaya

Mradi wa emBRACE hulenga kuboresha  jinsi  walioko ulaya huelezea wazo la unyumbukaji. Wakitumia mbinu za taaluma za maeneo kadhaa ambazo zinaunganisha na kushirikisha jumuia, mradi huu utakuza methodolojia za kuelezea namna unyumbukaji katika jamii inayokumbwa na maafa asilia unaweza kuelezewa,kufasiliwa na kupimwa.Indiketa za kupima unyumbukaji zitapendekezwa kutokana na uzoefu  na nadharia. Washika dau na wataalamu kadhaa watahusishwa katika vikundi mbalimbali vya kueneza maarifa.Jambo tofauti na mradi wa emBRACE ni  kwamba utatafuta watu na vikundi ambavyo kwa kawaida huwa havitambuliki:sio kwa nia ya kuwachunguza katika utafiti, mbali watakuwa kama washiriki na wataalamu kwa uwezo wao wenyewe (kwa mfano kupitia kubadilishana masomo na vikundi vya jamii shinani.


Utazamaji wa ardhi (kimetrolojia) katika uzuiaji na utawala wa vimelea vya malaria

Shabaha kuu ya mradi wa MALAREO ni kukuza teknolojia na kuanzisha uwezo wa kutazama ardhi (Earth Observation-EO) kwenye taratibu zilizomo Afrika Kusini za kutawala na kuzuia ueneaji wa vimelea.Ili kutimiza nia hii,ubadilishanaji wa maarifa pamoja na uwezo wa kufanya kazi utafanyika kwa njia mbili ((EU <-> SA).Kwa kufanya hivi mradi utachangia kuweko kwa tawi ambalo litasaidia katika kazi za kila siku za taratibu za kitaifa zinazolenga kuzuia malaria. Ili malengo ya mradi huu yatimizwe,itabidi kuweko na taaluma mbalimbali ambazo zinaambatana na ni madhubuti na kuwe na ushirikiano katika bara. MALAREO itatumia utafiti na uendelevu uliofanywa katika siku zilizopita wa kuzuia na kusimamia ueneaji wa vimelea vya malaria.Mradi utatumia,kama mfano wake, eneo la Lubombo ukishirikana kwa karibu na watakaofaidika kutokana na mradi huu.Madhumuni ya MALAREO yataitikia mahitaji ya watakaofaidika,na vilevile,kutilia nguvu ushirikiano wa GMES kama ilivyoelezewa katika ‘EU-South Africa Space Dialogue Joint communiqué.’


Kuboresha jinsi ya kutoa maonyo ya mapema dhidi ya ukame na uwezo wa kutabiri ili kuongezea nguvu za kuwa tayari na kuweza kufanya marekebisho barani Afrika

Madhumuni haswa ya DEWFORA ni kujenga muundo wa kuwezesha kutoa onyo la mapema na kuweza kuitikia kwa kupunguza athari za ukame barani Afrika.Muundo huu utajumlisha utazamaji na ukadriaji wa walioathirika, utabiri wa hali ya siku zijazo ,kutoa maonyo na kutawanya maarifa. DEWFORA inatarajia kuchangia kwa kuongezea nguvu zaidi katika namna ambavyo ukame unatabiriwa na jinsi maonyo na uwezo wa kuitikia unaweza kutolewa.DEWFORA itatoa mwongozo kuhusu jinsi marekebisho kutokana na ukame yanapaswa kufanywa na maeneo yanayopaswa kulengwa ili kuweza kuongezea unyumbukaji na kuboresha mbinu zilizoko za kukabiliana na kupunguza athari za ukame.


Mradi wa AfriCAN Climate

AfriCAN Climate ni mradi ulioundwa na timu ya mashirika 5 ya Afrika na 5 ya Ulaya,yakiwemo mashirika ya utafiti.  AfriCAN Climate Portal ni tovuti iliyoundwa upya ili kuwezesha mawasiliano kati ya wanaofanyia utafiti nyanja za mabadiliko katika tabia ya nchi na ili kuwezesha  kuigwa kwa methodologia bora zaidi.Kwenye tovuti hii washiriki wanaweza kuchangia maarifa kuhusu mada za utafiti zinazowavutia,kubainisha machapisho ,miradi na matukio yenye umuhimu zaidi;wanaweza kujadiliana na wahusika wengine wa jumuia ya AfriCAN na kuunda vikundi vipya vya kubadilishana mawazo na kuhojiana. Jumuia ya AfriCAN inawaalika watafiti,weledi,watunga sera,mashirika yasiyokuwa ya serikali,wanafunzi, mashirika mengine mbalimbali na wenye utaalamu katika suala la mabadiliko ya tabia ya nchi.Ungana nasi hapa tuweze kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu tatizo hili  barani Afrika na jinsi ya kupunguza athari  na kuweza kufanya marekebisho.


Muungano wa Afrika (AU) na Muungano wa Ulaya (EU)

Mnamo mwaka wa 2010 muungano wa Ulaya uliyochapisha wito wa mapendekezo yanayoshughulikia baadhi ya malengo ya Sayansi na Teknolojia ya "Afrika - EU Mkakati wa Ushirikiano", ukitilia mkazo "Maji na Usalama wa Chakula na" Afya Bora kwa Afrika "Mwaka wa 2011, miradi inayolenga masuala yanayohusiana na maji na ambayo ilifadhiliwa kupitia “wito wa Afrika” iliungana na kundi la Muungano wa Afrika (AU) na Muungano wa Ulaya (EU). Lengo la kundi hili ni kuwezesha ubadilishanaji wa habari na maarifa kati ya wanasayansi wa Afrika na Ulaya, kuchechemua uwezo wa kufanya kazi pamoja na kuongeza matokeo ya miradi kwa kufanya kazi pamoja. 

Vifaa 

Modeli ya ICTP, TRIeste ya magonjwa yanayosababishwa na vekta

VECTRI (http://www.ictp.it/~tompkins/vectri) ni modeli ya kihesabu inayoonyesha kusambaa kwa malaria, na hivyo kudhihirisha athari zinazotokana na ugeukaji katika tabia ya nchi na idadi ya watu. Modeli hii iliandikwa kuanzia mwaka wa 2011 na kutolewa rasmi katika warsha ya pili ya Afrika Mashariki iliyohusu mabadiliko ya tabia ya nchi katika chuo kikuu cha Addis Ababa mwezi Novemba 2011. Lengo la modeli hii haswa, ni kutoa chombo cha utafiti kitakachowezesha kuelewa kile ambacho kinasababisha kusambaa kwa ugonjwa wa malaria kinachoweza kutumika katika maeneo mbalimbali, lakini kwa hali thabiti ya kilometer 10 angani. 


Modeli ya magonjwa 

Modeli  ya magonjwa  pamoja na maelezo ya jinsi ya kutumia na mfano wa data sasa iko tayari na yaweza kupakuliwa kutoka tovuti ya QWeCI (Mshiriki wa Mradi wa Afya Bora ya Baadaye) http://www.liv.ac.uk/qweci/project_outputs/#d.en.241691.

DMC ni programu ambayo huwezesha kutolewa kwa modeli kadhaa za magonjwa, kwa mfano modeli iliyoundwa na wanasayansi wa chuo kikuu cha Liverpool inayowezesha ukadriaji wa ugonjwa wa malaria, pamoja na ile ya kukadiri homa ya bonde la ufa. Modeli hizi hutumika kwenye programu ya DMC na hutoa vielelezo kwa kutumia grafu. Lengo la programu hii ya DMC ni kuwezesha watumiaji kufanya modeli hizi katika  taasisi zao  mitaani wakitumia data zao za metorolojia kuchunguza na kuthibitisha matokeo kutokana  na vipimo vya mlipuko wa magonjwa (kuenea kwa ugonjwa wa malaria, idadi ya mbu walioambukizwa kilingana na modeli ya LMM). DMC pia yaweza kutumika kwa Windows, na Mac OS X.


Vifaa vya kufanya marekebisho dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi

Huwezo wa kutekeleza marekebisho kutokana na mabadiliko katika tabia ya nchi  ni changamoto; Kitakiwacho ni kuelewa, siyo tu  hatari zilizoko kwa sasa  na hatari za siku sijazo, lakini hasa kuelewa hali ya kiuchumi na kijamii ambayo miradi ya kurekebishwa itatekelezewa. Kuna mbinu kadhaa za 'kawaida' na vifaa mbalimbali vinavyoweza kutumiwa. Hata hivyo vifaa vipya vimeanza kutokea ambavyo  vinashurutisha  habari maalum kuhusu tabia ya nchi, ama kuunganishwa kwa habari ya tabia ya nchi na maamuzi yanayofanywa kuhusu marekebisho dhidi ya mabadiliko katika tabia ya nchi. ADx imeundwa kufanya kazi kama kifaa ambacho maamuzi mengi yatakayoleta manufaa huweza kuchaguliwa, kutumika na hata kulinganishwa. 

Taarifa

Shirika la Afya Duniani (Factsheets)

Malaria; http://www.who.int/mediacentre/factsheets/fs094/en/index.html

Homa ya bonde la ufa; http://www.who.int/mediacentre/factsheets/fs207/en/index.html

Kichocho; http://www.who.int/mediacentre/factsheets/fs115/en/index.html


Ujumbe kuhusu tabia ya nchi kwenye Mfumo wa Afya ya Uuma

CIPHAN imeanzishwa ili kutoa maarifa,methodologia,vifaa na data kwa wale wanaofanya kazi katika idara za afya ya uuma ili kuwawezesha kukabiliana na magonjwa yanayosababishwa na mabadiliko katika tabia ya nchi, na hivyo kuwezesha kuweko na matokeo bora katika kukabiliana na magonjwa kama hayo. CIPHAN huwa kama chanzo cha kuelekeza wanaojifunza kwenye maandishi mengine yenye maarifa, na pia ni chombo asili chenye mazoezi ya aina mbalimbali ya kujifunza.Maktaba ya tovuti hii pia ina orodha ya habari zilizotolewa ili kumpa msomaji nafasi ya kufanya uchunguzi zaidi.

Read 51523 times Last modified on Dinsdag, 11 November 2014 14:48
Translate